Vodacom na escrow

Vodacom na escrow

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16


Kuna promosheni kubwa kutoka Vodacom inayoendelea hivi sasa ambayo nadhani wengi tumeona matangazo yake. Inaitwa "mamilioni ya jay" au "jaymillions". Katika tangazo lake linalochezwa na muigizaji maarufu nchini Tanzania, Hillary Daudi au maarufu "zembwela", ‘bwana j', ananukuliwa akisema: "mimi ndio j, ….nimeamua kugawa mihela yangu". Promosheni hii ingetoka wakati wowote ule kabla ya kikao cha bunge lililopita basi mawazo yangu haya yote yasingekuwa na maana. Ila kwa sababu limetoka muda huu naomba niwashirikishe mawazo yangu juu ya nini hasa muktadha wa tangazo tukiweka pembeni malengo ya kibiashara ya kampuni ya Vodacom. Niweke wazi kuwa sina maslahi yoyote ya ziada ukiacha uteja wa voda na mitandao mingine. Hii blog post ni mawazo yangu na sio tangazo la biashara. Sasa tuendelee.

[video=youtube_share;pQAdvCV6NNY]http://youtu.be/pQAdvCV6NNY[/video]​

Jina na kabila la mhusika:
Kutoka kwenye tangazo, hakuna shaka kuwa "bwana j" ni mhaya. Lafudhi yake inadhihirisha hilo. Mhusika halisi katika sakata linaloendelea sasa, anayesemekana "kugawa" fedha zake pia ni mhaya na jina lake linaanzia na herufi j. coincidence mbili? wangeweza kutumia lafudhi ya kabila lingine na vile vile jina lingine, kama bado hujakubali basi tuendelee.

Kiasi cha zawadi:
Katika sakata la akaunti ya escrow, bwana j anaripotiwa kugawa ‘zawadi' za mamilioni mpaka mabilioni ya pesa, sio jambo la kushangaza kwa mtu aliyeita bilioni 121 kuwa ni ‘vijipesa vya ugoro'. Kwa upande wa pili, ‘Bwana j' wa Vodacom naye pia anagawa pesa nyingi sana kuliko kawaida. Promosheni hii ya ‘mamilioni ya bwana j' inasemekana kuwa ndio promosheni kubwa kuliko zote za michezo ya kubahatisha nchini Tanzania. Katika siku mia moja tu, ‘bwana j' atagawa zawadi za thamani ya bilioni 30 za Tanzania. Zawadi ya juu ikifikia milioni 100 kwa siku! Hivyo ‘bwana j' wa Vodacom ni bilionea vile vile kama yule bwana j wa akaunti ya escrow.

Utaratibu wa kushinda/Jinsi ‘bwana j' anavyogawa fedha:
Tofauti na utaratibu wa promosheni zilizozoeleka ambazo mara nyingi mshiriki anashindana, katika hii ya "bwana j", Vodacom wameleta utaratibu mpya, "kucheki". Ingawa bado utatakiwa kutuma ujumbe kwa namba fulani fulani, kimsingi "haushindani", bali unachofanya ni "kucheki" kama ‘bwana j' amekuingizia fedha kwenye akaunti yako.Vinginevyo huwezi jua kuwa una hela.
Utaratibu huu umefanana sana na na namna ambavyo wanaotajwa kuwa wanufaika wa bwana j wa ukweli walivyopata "mgao wao". Kwa mfano bwana Emmanuel Ole Naiko aliyetajwa kwenye ripoti ya bunge, hakujua kama amepata "mgao" mpaka pale aliposhtuliwa na ripoti za magazeti, na hivyo kumlazimu "kucheki" akaunti yake kama ni kweli.

"He, however, told The Citizen that he did not know at first that there was such an amount in his account until he checked. "I rarely used this account and immediately I got notice of the deposit I went to inquire the source."
Chanzo: Ole Naiko speaks out on his share of escrow billions - National - thecitizen.co.tz

"Ole Naiko alisema jana kuwa baada ya kutajwa kwenye ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), bungeni Novemba 28, mwaka huu ndipo alipokwenda kuhakiki na kubaini kuwa ni kweli fedha hizo zipo."
Chanzo: Ole Naiko ajitetea: Sikujua kama nimewekewa mamilioni - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Kama ulikuwa na uhakika bwana j wa ukweli alikuwa na namba ya akaunti yako, basi wewe kazi yako ilikuwa kucheki tu. Kwa vile ‘bwana j' wa vodacom tayari anazo namba za wateja wote wa vodacom, unachotakiwa kufanya ni kucheki tu kama amekuingizia "mgao". Mfumo ni ule ule. Hakuna shaka kuwa tangazo hili linalenga sakata la escrow.

Changamoto kwa matangazo ya mitandao mingine:
Tumezoea kuona mitandao ya simu ikishindanisha matangazo yao kwa ubunifu mkubwa wa kupigana vijembe. Mfuatiliaji wa matangazo atakumbuka mashindano ya kibito, kibajaj na lile basi kubwa ambalo wateja walikuwa ‘wanahamia'. Mara nyingi huwa wanashindana kwa kutumia theme ile ile aliyoanzisha mmoja wao. Haitakuwa ajabu kuona mtandao mwingine umetoa tangazo kwa kutumia theme hii hii ilikotokea ‘mamilioni ya j'. Binafsi nashauri mtandao mwingine uandae promosheni ya kugawa misaada kwa mashule mbalimbali itakayokuwa inagawiwa na muigizaji mwanamke, mwembamba, mwenye nywele fupi au anayevaa kilemba, mwenye lafudhi ile ile ya ‘bwana j' wa voda bila shaka, itakayokwenda kwa jina la "madawati ya mama prof", "school fees from mama T" au kitu kama hicho, mnaonaje? Ni wazo tu.
Au labda mitandao pinzani ifanye subira, wakisubiri hatma ya sakata halisi.....labda tangazo lao likawa linahusu wao wakichekelea 'bwana j' kukamatwa.....
 
Nimejiuliza sana jana, hii promosheni kwanini waiite Jay na Si voda au majina mengine. Isije kuwa haya mamilioni kawekeza James Rugemalila kupitia Vodacom, huu ni wakati wa kujua kama James hana hisa zake Vodacom kama anazo basi kuna uwezekan Vodacom inatumiwa na mafisadi.
Haiingii akilini kwann iitwe Jay(James Rugemalila).
 
Back
Top Bottom