Habari wadau.
Nimekua na wazo la mda mrefu nikadhani huwenda Vodacom watakua wanawaza the same ila naona bado.
Simu zetu zimekua ndio Bank zetu za karibu, pamoja na huduma za kipesa zinazotolewa kama vile Mikopo na Deposit ,nimeona iko haja ya Mpesa kufika mbali kidogo na kutuwekea "Mpesa Fixed Account." au vyovyote vile watakavyopendelea kuiita.
Kuna wakati mtu unakua na Pesa kwenye Account ya Mpesa ila Malengo ya Pesa yenyewe unakuta bado siku hazijafikia, ni rahisi kujiwekea katika Fixed Accont zaidi,Mfano wanakua na Account za kuanzia Wiki mbili , hadi Mwezi.
Hii itasaidia sana kutupunguzia Matumizi yasiyo ya msingi na kuepuka vishawishi vya hapa na pale katika matumizi ya Pesa kwenye Account zetu.
Ahsanteni
Pesa ni Mpesa.
Nawasilisha.