Miaka sita iliyopita nilifika goba. Kwa kweli palikuwa nyuma sana. Ila kwa sasa nipo hapa goba, mda huu wa saa mbili usiku, kwa kweli pamekucha. Hapa kuna barabara nne muhimu. Moja inaelekea makongo juu ambayo ina magari mengi. ya pili inaelekea mbezi beach tangi bovu. ya tatu inaelekea madale, wazo mpaka tegeta, ya nne inaelekea mbezi liusi. Nakutonya tu mjasiria mali, wahi ufanye survey uwekeze mapema kabla mambo hayajawa makubwa zaidi kwani barabara ya lami ipo karibu kujegwa. Goba ipo juu kijeografia, hali ya hewa ni nzuri kiama.