Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Sera ya serikali ya kulinda viwanda vya ndani ina nia njema ya kukuza uchumi na kuongeza ajira lakini, yapo mazoea ya viwanda vyetu kuzalisha bidhaa zisizo na ubora. Serikali kupiga marufuku bidhaa za nje kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani panahitajika umakini mkubwa sana. Hofu yangu ni kuwa tusije tukarudi enzi ya Nyerere ambapo tulilazimika kununua bidhaa zisizokuwa na ubora wowote, mfano: viberiti visivyowaka, sabuni zinazoharibu mikono, mafuta ya kula machafu, sukari iliyochanganywa na takataka, mishumaa isiyowaka, betri za redio zinazovuja kabla ya kutumika, matairi ya magari yalikuwa yanapasuka siku ya kwanza tu, mashati ya shule yalikuwa kama yameshonwa na mataahira nk..nk. Ingekuwa busara sana kama serikali ingelinda bidhaa za ndani dhidi ya zile za nje kwa kuweka viwango tofauti vya kodi na ushuru halafu waachwe watumiaji waamue kuliko kulazimisha kutumia bidhaa za ndani hata kama hazikidhi ubora..