Viwanda vya zamani au majalala?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,834
Reaction score
15,626
Kumekuwa na watu wengi wakifikiri serikali kweli inachukuwa viwanda vya zamani. Lakini viwanda wanavyosema ni bora wauze tu kiwanja kwenye mnada kwasababu zifuatazo

1. Hazina hata mashine moja nyingi na zimebaki kuwa majalala
2. Haziko sehemu maalumu za kiwanda hivyo maeneo mengi hayawezi kukuzwa
3. Ni garama sana kutoa matakataka na kusafisha upya kuliko kuanza upya kwenye kiwanja kipya
4. Masoko yamebadilika mfano kiwanda cha ngozi sasa hakuna wafugaji wengi Mwanza badaya yake ingefaa kiwanda kiwe karibu na Dododoma, Arusha au Morogoro kwenye mifugo
5. Mtaji wa kuanzisha hivi viwanda ni sawa na kuanza upya na vingi hata location haifai tena.
6. Ushindani wa sasa ni tofauti sana na dunia ya nyerere. Tujiulize nani atavaa bora kwa miaka ya sasa... kwa mfano

Hivyo badala ya kufungua viwanda tu bila mpango ni lazima tujiulize je serikali inataka kurudi kwenye biashara au itafanya minada upya? na mwekezaji kwenye ana pata kiwanda au dempo ya takataka na kiwanja?
 
Akimaliza viwanda ahamie kwa nyumba za serikali......
 
Bidhaa.za kitania vs bidhaa za nje

1)blue band.vs tanbond
2)kimbo vs pride
3)samli kccc vs supaghee
4)Colgate vs bonamed
Afadhali hata hawa wanashindana sokoni
5)vaseline vs vestline
6) omo vs foma
 
Huelewi kitu wewe bora unyamaze tu... hivyo viwanda vinatakiwa vifufuliwe so Serikali haijihusishi na Biashara bali itawapa watu wenye nia na uwezo wa kuviendesha kwa gharama yao wenyewe ili viwe active na uzalishaji ufanyike na raia wapente ajira na serikali ipate kodi kwa bidhaa zitakazo zalishwa na kodi za mishahara ya wafanyakazi watakaofanya kazi hapo na pia pesa za michango ya mafao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…