Hili ni tatizo, tena tatizo kubwa, hawa jamaa wanachafua mazingira kwa uchafu wa bidhaa zao napi haja ndogo kwenye chupa ambazo zinatupwa hovyo, au pembezoni mwa nyumba za jirani au majengo ya jirani yalioyopo.
Lakini cha kujiuliza huu ushuru wanaochukua nani ananufaika nao? serikali ya mtaa, kata au halimashauri husika? kama halimashauri zingebuni utaratibu mzuri muda wa jioni katika vituo vikubwa naamini wangenufaika mno, hivi sasa kila kituo ikifika jioni ni soko, nenda ubungo, mwenge, buguruni, tazara sijui gongo la mbali mboto wapi....
Unashindwa hata kuegesha kagari kako ukapata huduma za jamii katika eneo hilo... Nafikiri hizi alimashauri za kata na miji zifanye jambo la maana...