Vituo vya Afya..

Hamud1988

Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
14
Reaction score
10
Unapereka mgonjwa kituo A cha afya kinachomilikiwa na serikali saa 10 jioni unaambiwa mrete kesho tumefunga, unampereka kituo B kinachomilikiwa na serikali anapewa Huduma tena nzuri..

Naomba mwenye ufahamu na sheria na kanuni za afya anielimishe mwisho wa kupereka wagonjwa kituo cha afya ni saa ngapi.?
 
Si kweli mkuuu..ulienda zahanati(dispensary),kituo cha afya kinaitwa health centre....
 
Pereka, pereka,
 
Muundo wa zahanati huwa ni kufanya kazi masaa 8 kwa siku 5 tu kwa wiki, siku za wikiendi na siku kuu ni siku za mapumziko kwa watumishi wake.

Mtumishi wa zahanati asipopumzika jumamosi na jumapili maanayake atafanya kazi mwezi nzima bila kupumzika jambo ambalo halipo

Mtumishi wa zahanati asipofunga kituo cha kazi saa 9 na 30 mchana maana yake anaweza fanya kazi masaa 24 nacho ni kitu kisicho kuwepo.

Mamlaka husika zimezifanya zahanati kuwa ni sehemu ya kutibu wagonjwa wenye matatizo kidogo na ndio maana kunakuwa na watumishi wachache sana pengine hata wanne tu hivyo sio rahisi kupangiana shift ili wafanye kazi masaa 24.

Hatahivyo kwakuzingatia wagonjwa waliokatika hatari ya kupoteza maisha, au kupata ulemavu ikiwa watachelewa kupata huduma, mamlaka husika zimeweka utaratibu wa walau mtu mmoja anashika zamu kwa ajili ya kutoa duma ya kwanza na kuwapa rufaa wagonjwa hao walio katika hari tete. Mtumishi huyo hufanya kazi hiyo akiitwa kutokea nyumbani kwake kwani huwa anakuwa ameweka jina na namba yake ya simu katika mlango wa zahanati.

Mkitaka huduma ya uhakika siku za wikiend na jioni baada ya saa 9 na 30 muende kituo cha afya wanapolaza wagonjwa.
 
Hii ni forum ya picha siyo insha.
 
Ahsante mkuu

its ALMIGHTY's wishes that we are still alive
 
Nmefatilia kituo husika nmesoma bango Lao upya kimeandikwa KITUO CHA AFYA tena wakaweka na MUDA WA KAZI 24Hrs

its ALMIGHTY's wishes that we are still alive
 
Nadhani uko kwenye nafasi sahihi katika idara ya afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…