Tukio namba moja nadhan,liliwah kutokea nikiwa Tanga. Natoka bush huko, naenda Tanga town, kwa magara ya nauli buku tatu. Sasa tukiwa ktk ya vijiji vya pori ikaibuka ubishani ktk ya dada mmoja na kondakta.
Kimuonekana dada alikuwa na ka umbili kadogo tu, lakini anatema cheche balaaaa. Mabishano yalivyoendelea dada akasema, mnishushe sehem flan, yule konda akasema huko unakotaka hakuna kituo, Vituo vya kule pori viko mbalimbali kdgo. Konda alisem kumkomoa tu, maana hushusha na kupakia popote wanapopenda sema ni aliamua hivo tu
Dada alikuw na mizgo yake kafunga furush kwa kanga tu kama sikosei, yaan kafunga ki simplo simple tu, akasema aiseee NITAZIMA GARI SASA HIVI, SAFARI IISHE HAPA Konda akaendelea kubishana ,kuna watu wakamtonya, kuwa WATU WA KIJIJ HIKI, WASIKIE TU, KUNA MAFUNDI HAPO.