Vituko vya CCM kwa Wilson Mukama ndio Utani kwa CHADEMA kwa Vincent Mashinji.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Vituko vya CCM kwa Wilson Mukama ndio Utani wa CHADEMA kwa Vincent Mashinji.

Vituko hivi na utani huu wakati CCM alipotolewa MTU mwenye ushawishi mkubwa Mzee Yusuf Makamba, wengi WA wana CCM walifurahi sana na hii ni kwa kuwa Mzee alikuwa hashikiki kimkakati na kiufundi kutokana na Karama zake na ndio maana aling'aa sana kupita wote chama kizima. Njia ya kumzima ilikuwa ni kumuondoa kisaikolojia Ukatibuni Mkuu WA Chama. Na hapo ndipo aliteuliwa Wilson Mukama kuwa Katibu Mkuu WA CCM.

Ukweli una uuma, Mkama hakuna chochote cha maana alichokifanya kwa CCM zaidi ya kuongea na media Mara kwa Mara. Na hii ilikuwa ni njia safi kwa wanasiasa ndani ya CCM ambao ni waoga kufunikwa kisiasa, na walimpenda sana. Lakini kwa muda mfupi wakashituka chama kitapigwa chini na wapinzani, hawakuona haja ya kumrudisha Mzee Makamba maana wanamjua makali yake, ndipo wakamuibua Kinara WA utekelezaji anayoyasema Ndugu Abraham Kinana. Na hapo ndipo CCM ikasimama tena upya.
HAWA ndio wana CCM oyeeeeeeeeee.

Kwao Makamanda WA Chadema ili hali wanajua nguvu kubwa aliyonayo Dr. Wilbrod Slaa na ushawishi wake ndani na nje ya chama kama Katibu Mkuu, wengi walimpenda sana maana alisababisha mabadiliko mengi ndani ya chama na nje ya chama. Lakini kwa tamaa ya watu wapya hasa kipindi cha uchaguzi Mzee Slaa alionekana hana thamani tena, Dr. Slaa akaamua kukaa pembeni kuona ngoma za kijogori zinavyo chezwa. Hata hivyo CHADEMA wakakaa kama Kamati Kuu wakamteua Mh. Mashinji kuziba pengo la Slaa. Huwezi amini tangu wamemteua Katibu Mkuu wao mpya hakuna cha maana chochote anachofanya zaidi ya kuiangamiza Chadema, chama kimekuwa na mikosi kuliko hapo awali. Wanafikiri wanafanya kazi kumbe wanadondoka chini bila kujijua wakifarijiana kwa kupokea wanachama wabunge wastaafu.

Nachokiona hapa ya Mukama kukaa muda mfupi kwenye Ukatibu Mkuu ndio huenda yakamkuta Mashinji. Je, Slaa atarudishwa na kuijenga upya Chadema au kuna kifaa kipya kimeandaliwaa. Yetu ni macho na masikio kujua nini kitafuata kuiokoa Chadema ya matamko hewa yanayopingwa na watawala. Mimi Deogratius Kisandu naiona Chadema kuwa mbovu kama haitabadili Mtazamo wake, lakini naiona Chadema kuwa nzuri kama itajijenga upya. Mafanikio ya chama cha Chadema hayataletwa na Mh. lowasa wala Mh. Mbowe Bali ni mabadiliko chanya ndani ya chama ndio yataiinua Chadema.

Nawatakia Kheri ya nzuri ya kumaliza mwaka 2016 na kuanza mwaka mpya 2017.

deogratius Nalimi Kisandu.
30 Desemba 2016.
KAHAMA-Tanzania
 
Kuna ukweli Fulani.Katibu Chadema anapwaya
 
Mbona naona ni tofauti.Mukana na Makamba Nani alimpisha mwenzie
 
Back
Top Bottom