Vituko mitandaoni. Tupia chako

Watu wataongezeka, wafugaji holela wataongezeka na hivyo mifugo itaongezeka mara dufu.
Miti itakatwa yote ili kujenga miundombinu ya ufugaji, vyanzo vya maji vitakaushwa vyote kutokana na kwato za wanyama na uharibifu mwingine wa mazingira.
Tanzania hatimaye itakuwa nchi ya Jangwa. Jangwa kubwa litachukua nafasi hasa kwenye mikoa ambayo hivi sasa ina misitu minene na ambayo ndiyo inayowindwa na wavamizi wenye mifugo wengi.
Morogoro, Lindi, Iringa, Ruvuma,Rukwa, Katavi na Tanga.
Mungu ibariki Tanzania.
Ila nashukuru kwamba mwaka 2100 sitakuwepo, ingawa nina hakika kizazi cha wakati huo kitayasimanga makaburi yatu kwa madhara tuliyoitendea nchi hii kiasi cha kuwaachia janga la ukame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…