Vituko mitandaoni. Tupia chako

JINSI YA KUIBA NYAMA KWENYE HOT POT
01.Ingia jikoni,angalia kushoto na kulia Kama Kuna mtu anakuja

02.Angalia mkao wa kijiko kimekaaje ili mda wakuondoka ukiache vile vile kilivyokaa usikigeuze,usifanye kosa


03. Fungua hot pot pole pole ,usiache mfuniko upige kelele au uanguke(utashtukiwa)

04.Hesabu vipande vya nyama hakikisha vipo kuanzia vitano na kuendelea maana kama vipo chini ya vitano ni rahisi mama kujua vipande vilivyopungua.Sasa ni mda wa kuchukua mnofu anza kuutafuna
..lakini Kama vipande viko chini ya vitano basi chukua kimoja kimoja na kung'ata robo afu kirudishe chukua kingine fanya hivyo hivyo kwa minofu yote(unang'ata kidogo unaacha kidogo)..

05.wakati unakula ,simamisha masikio yako vzr kusikia Kama Kuna mtu anakuja(atakufuma),usiruhusu mchuzi ukudondokee kwenye nguo au kudondoka chini,na Kama chuzi utakudondokea wahi haraka fua nguo..na ondoa ushahidi wowote jikoni

06.Baada ya kula nawa mikono kwa sabuni na uinuse mara 6 Kama unahisi harufu Bado ipo nawa tena na tena..

07.Weka viganja kwa kuziba mdomo afu pumua kusikia Kama harufu ya nyama inatoka kinywani


Usiwe na wasi wasi kuhusu Hilo,chukua tangawizi au au limao tafuna kuondoa harufu

08.sasa toka jikoni Kama mtakatifu,maana uko salama


Kesho ntafundisha jinsi ya kumuiba mke wa mtu.
 
lakini Kama vipande viko chini ya vitano basi chukua kimoja kimoja na kung'ata robo afu kirudishe chukua kingine fanya hivyo hivyo kwa minofu yote(unang'ata kidogo unaacha kidogo)..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
So sad. Imenikumbusha mbali sana. ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…