Watu 7 (Wawili wana asili ya #Asia) wanashikiliwa baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) kukamata Kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya #heroin (Kg. 2,180.29) na #methamphetamine (Kg. 1001.71) katika Mikoa ya #Dar na #Iringa (Wilaya za #Kigamboni, #Ubungo #Kinondoni na #Iringa) kati ya Desemba 5 na 23, 2023.
Taarifa ya #DCEA imeeleza kuwa Ukamataji huo umehusisha kiasi kikubwa cha #DawaZaKulevya ambacho hakijawahi kukamatwa katika historia ya #Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya
Taarifa hiyo imefafanua zaidi kuwa dawa hizo zilizokuwa kwenye vifungashio vya bidhaa zenye chapa mbalimbali za #Kahawa na Majani ya Chai, endapo zingefanikiwa kuingia Mtaani zingeweza kuathiri zaidi ya watu 76,368,000 kwa siku.
Soma
Dawa za Kulevya: Serikali yawatia Mbaroni Mapapa 7 wa Unga
#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability
Sent using
Jamii Forums mobile app