Vitu vitano (5) ambavyo mwajiri wako hataki wewe ujue, Ili aweze kukutumia vizuri

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,915
3,407
Mfumo wa kuajiri na kuajiriwa ni moja ya mifumo ambayo imekuwa inatumiwa na watu kuongeza ufanisi kwenye kazi zao, kwa wale wanaoajiri na pia kujipatia kipato, kwa wale anaoajiriwa. Huu ni mfumo ambao ulianza baada ya mapinduzi ya viwanda na hivyo uhitaji wa wafanyakazi ukawa mkubwa. Mfumo huu ulikua kwa kasi kadiri viwanda vilivyokuwa, lakini ukaanza kupoteza nguvu kadiri teknolojia ilivyoendelea kukua.

Na mpaka sasa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo mfumo wa ajira unavyozidi kuwa dhaifu katika kutengeneza kipato cha uhakika kwa wale wanaoajiriwa.

Ili mfumo huu wa ajira uende vizuri kuna mambo ambayo huwa hayawekwi wazi, iwe ni kwa kutokuelezwa kwa ukweli au kutojadiliwa kabisa. Hii ni kwa sababu ukiangalia kwa undani uhusiano kati ya mwajiri na mwajiriwa siyo uhusiano ambao kila mmoja ananufaika sawa. Kuna ambaye ananufaika zaidi ya mwenzake. Hivyo bila ya kutengeneza mazingira ya watu kukubaliana na hilo ni vigumu kuendesha mfumo huu.

Leo kupitia makala hii tutajifunza vitu vitano ambavyo mwajiri wako hataki wewe uvijue ili aweze kukutumia vizuri. Tutajifunza pia hatua ya kuchukua ili uweze kununua uhuru wa maisha yako. karibu sana tujifunze kwa pamoja ili tuweze kuboresha maisha yetu.

1. Mwajiri anakutumia wewe kufikia ndoto yake.

Hili hatakuambia wazi wazi, lakini ndiyo kitu anachofanya. Mwajiri wako anakuwa na ndoto yake kubwa, ila sasa anakuwa hana ujuzi na muda wa kutosha wa kufanya kila kitu yeye peke yake. Na hivyo anaangalia ni watu gani ambao hawana ndoto kubwa za maisha yao, au ni watu gani wana ndoto lakini anaweza kuziua? Anatangaza nafasi na wanajitokeza watu. Anapata ambao hawana ndoto na anawatumia, na kuna ambao wana ndoto anaowapata ila anahakikisha ndoto zao zinakufa kwa sababu tutakayoiona hapa.

2. Mwajiri wako siyo rafiki yako.

Haijalishi anakuonesha anajali kiasi gani, au mazingira gani ya kirafiki anakuonesha, mwajiri wako siyo rafiki yako, yeye anajua hilo ila hataki wewe ujue. Anataka wewe uendelee kumwona kama rafiki ili uendelee kutekeleza ndoto yake. Lakini mambo yanapokuwa magumu upande wake, pale inapotokea huzalishi kama alivyokuwa anategemea, hana namna bali atakuacha nakuajiri mtu mwingine. Marafiki wa kweli hawawezi kuachana kwa sababu kama hiyo. Jua wazi ya kwamba mwajiri wako au bosi wako siyo rafiki yako, kinachowaleta karibu ni ule mchango ulionao kwenye ndoto yake, ukikosa mchango huo hana tena muda na wewe.

3. Siyo lengo la mwajiri wewe utajirike.

Sasa ukitajirika nani ataendelea kumfanyia kazi zake. Hii ndiyo sababu mwajiri anakulipa kiasi ambacho utaweza kuendesha maisha yako ya kawaida na ili uendelee kuendesha maisha hayo ni lazima uendelee kumfanyia kazi. Hakupi kile unachotaka wewe ili ufanikiwe, bali anakupa kile ambacho kitakutosha kwa wakati tu, lakini uendelee kumtegemea kwa kipato. Mwajiri wako atakupa sababu nyingi kwa nini kipato ni kidogo, lakini kwa undani sababu halisi ndiyo hiyo.

4. Kwamba unaweza kujitegemea mwenyewe.

Kitu kingine ambacho mwajiri wako hataki ujue ni kwamba unaweza kujitegemea wewe mwenyewe. Anataka uone kwamba maisha yako hayawezi kwenda bila yeye na hapa ndiyo anakuwa na nguvu kubwa ya kukulazimisha ufanye chochote. Kwanza anaanza kutengeneza utegemezi huu kidogo kidogo na kadiri unavyokaa kwenye ajira ndivyo unavyopoteza kabisa kujiamini na kuona huwezi peke yako. ukishafikia hatua hii yeye anafurahi kwa sababu ana uhakika wa kutimiziwa ndoto yake.

5. Anakutegemea sana wewe.

Kitu kikubwa ambacho mwajiri wako hataki wewe ujue ni kwamba yeye anakutegemea sana wewe ili aweze kufikia ndoto zake. Na hataki kabisa ujue hili kwa sababu litamharibia mipango yake. Na ndiyo maana anatengeneza utegemezi na kukupa kiwango kidogo ili usahau utegemeze wake kwako wewe.

Ufanye nini?

Ajira zina changamoto nyingi, na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo changamoto zinavyozidi. Kipato cha ajira kimekuwa hakitoshelezi, unakuwa na madeni na huwezi kuiona kesho yako.

Hatua pekee ya wewe kujitoa kwenye hali hii ni kuanza kutengeneza hali ya kujitegemea ukiwa bado umeajiriwa. Na moja ya njia za kufanya hivyo ni kuanzisha biashara au kuwa mwekezaji. Kwenye kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, kuna mambo yote muhimu kwako wewe mwajiriwa unatakiwa kuyajua ili kuweza kununua uhuru wako. Pata kitabu hiki na ukisome utaona hatua za kuchukua. Kitabu ni softcopy yaani pdf na unaweza kusomea kwenye simu yako au kompyuta yako. gharama ya kitabu ni shilingi elfu kumi. Kupata kitabu hiki tuma fedha kwenye namba 0717396253 au 0755953887 majina Amani Makirita na kisha tuma emaila yako au ujumbe kwenye wasap kwenye namba 0717396253 kisha utatumiwa kitabu.

Anza kununua uhuru wako ukiwa bado umeajiriwa, usikubali kuendele akudanganywa tena na mwajiri wako.

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz
 
Atawezaje?kwa ufupi hukuelezea ni kwa njia gani mwajiri ataziua ndoto zangu?Mfano hapa :UNAWEZA KUJITEGEMEA MWENYEWE ni njia gani anatumia kuhakikisha siwezi kujitegemea bila yeye??ungeelezea point za msingi vinginevyo bado umetuachia maswali.
 
Mimi nijifunza huko nyuma kama ifuatavyo

Income (I) = Consumption (C) + Savings (S)
Savings (S) = Investment.

Niliajiriwa miaka 16 lakini kwa kutumia formula tajawa hapo nimeweza kufungua biashara yangu na mimi nina takribani wasaidizi 10 miongo mwao wahitimu wa chuo kikuuu ni 8. Hawa wasaidizi nawachukulia kama wabia kwenye biashara yangu na hata maamuzi mengi wao sehemu ya hayo maamuzi.

Siku zote mwajiriwa ukifanisha malengo ya mwajiri na ya kwako yanafaniwa labda huyo mwajiri awe na roho mbaya sana.
 
Mfumo wa kuajiri na kuajiriwa ni moja ya mifumo ambayo imekuwa inatumiwa na watu kuongeza ufanisi kwenye kazi zao, kwa wale wanaoajiri na pia kujipatia kipato, kwa wale anaoajiriwa. Huu ni mfumo ambao ulianza baada ya mapinduzi ya viwanda na hivyo uhitaji wa wafanyakazi ukawa mkubwa. Mfumo huu ulikua kwa kasi kadiri viwanda vilivyokuwa, lakini ukaanza kupoteza nguvu kadiri teknolojia ilivyoendelea kukua.

Na mpaka sasa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo mfumo wa ajira unavyozidi kuwa dhaifu katika kutengeneza kipato cha uhakika kwa wale wanaoajiriwa.

Ili mfumo huu wa ajira uende vizuri kuna mambo ambayo huwa hayawekwi wazi, iwe ni kwa kutokuelezwa kwa ukweli au kutojadiliwa kabisa. Hii ni kwa sababu ukiangalia kwa undani uhusiano kati ya mwajiri na mwajiriwa siyo uhusiano ambao kila mmoja ananufaika sawa. Kuna ambaye ananufaika zaidi ya mwenzake. Hivyo bila ya kutengeneza mazingira ya watu kukubaliana na hilo ni vigumu kuendesha mfumo huu.

Leo kupitia makala hii tutajifunza vitu vitano ambavyo mwajiri wako hataki wewe uvijue ili aweze kukutumia vizuri. Tutajifunza pia hatua ya kuchukua ili uweze kununua uhuru wa maisha yako. karibu sana tujifunze kwa pamoja ili tuweze kuboresha maisha yetu.

1. Mwajiri anakutumia wewe kufikia ndoto yake.

Hili hatakuambia wazi wazi, lakini ndiyo kitu anachofanya. Mwajiri wako anakuwa na ndoto yake kubwa, ila sasa anakuwa hana ujuzi na muda wa kutosha wa kufanya kila kitu yeye peke yake. Na hivyo anaangalia ni watu gani ambao hawana ndoto kubwa za maisha yao, au ni watu gani wana ndoto lakini anaweza kuziua? Anatangaza nafasi na wanajitokeza watu. Anapata ambao hawana ndoto na anawatumia, na kuna ambao wana ndoto anaowapata ila anahakikisha ndoto zao zinakufa kwa sababu tutakayoiona hapa.

2. Mwajiri wako siyo rafiki yako.

Haijalishi anakuonesha anajali kiasi gani, au mazingira gani ya kirafiki anakuonesha, mwajiri wako siyo rafiki yako, yeye anajua hilo ila hataki wewe ujue. Anataka wewe uendelee kumwona kama rafiki ili uendelee kutekeleza ndoto yake. Lakini mambo yanapokuwa magumu upande wake, pale inapotokea huzalishi kama alivyokuwa anategemea, hana namna bali atakuacha nakuajiri mtu mwingine. Marafiki wa kweli hawawezi kuachana kwa sababu kama hiyo. Jua wazi ya kwamba mwajiri wako au bosi wako siyo rafiki yako, kinachowaleta karibu ni ule mchango ulionao kwenye ndoto yake, ukikosa mchango huo hana tena muda na wewe.

3. Siyo lengo la mwajiri wewe utajirike.

Sasa ukitajirika nani ataendelea kumfanyia kazi zake. Hii ndiyo sababu mwajiri anakulipa kiasi ambacho utaweza kuendesha maisha yako ya kawaida na ili uendelee kuendesha maisha hayo ni lazima uendelee kumfanyia kazi. Hakupi kile unachotaka wewe ili ufanikiwe, bali anakupa kile ambacho kitakutosha kwa wakati tu, lakini uendelee kumtegemea kwa kipato. Mwajiri wako atakupa sababu nyingi kwa nini kipato ni kidogo, lakini kwa undani sababu halisi ndiyo hiyo.

4. Kwamba unaweza kujitegemea mwenyewe.

Kitu kingine ambacho mwajiri wako hataki ujue ni kwamba unaweza kujitegemea wewe mwenyewe. Anataka uone kwamba maisha yako hayawezi kwenda bila yeye na hapa ndiyo anakuwa na nguvu kubwa ya kukulazimisha ufanye chochote. Kwanza anaanza kutengeneza utegemezi huu kidogo kidogo na kadiri unavyokaa kwenye ajira ndivyo unavyopoteza kabisa kujiamini na kuona huwezi peke yako. ukishafikia hatua hii yeye anafurahi kwa sababu ana uhakika wa kutimiziwa ndoto yake.

5. Anakutegemea sana wewe.

Kitu kikubwa ambacho mwajiri wako hataki wewe ujue ni kwamba yeye anakutegemea sana wewe ili aweze kufikia ndoto zake. Na hataki kabisa ujue hili kwa sababu litamharibia mipango yake. Na ndiyo maana anatengeneza utegemezi na kukupa kiwango kidogo ili usahau utegemeze wake kwako wewe.

Ufanye nini?

Ajira zina changamoto nyingi, na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo changamoto zinavyozidi. Kipato cha ajira kimekuwa hakitoshelezi, unakuwa na madeni na huwezi kuiona kesho yako.

Hatua pekee ya wewe kujitoa kwenye hali hii ni kuanza kutengeneza hali ya kujitegemea ukiwa bado umeajiriwa. Na moja ya njia za kufanya hivyo ni kuanzisha biashara au kuwa mwekezaji. Kwenye kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, kuna mambo yote muhimu kwako wewe mwajiriwa unatakiwa kuyajua ili kuweza kununua uhuru wako. Pata kitabu hiki na ukisome utaona hatua za kuchukua. Kitabu ni softcopy yaani pdf na unaweza kusomea kwenye simu yako au kompyuta yako. gharama ya kitabu ni shilingi elfu kumi. Kupata kitabu hiki tuma fedha kwenye namba 0717396253 au 0755953887 majina Amani Makirita na kisha tuma emaila yako au ujumbe kwenye wasap kwenye namba 0717396253 kisha utatumiwa kitabu.

Anza kununua uhuru wako ukiwa bado umeajiriwa, usikubali kuendele akudanganywa tena na mwajiri wako.

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Upo sahihi ila kwa kulipia kitabu kwa m-pesa ndo inshu,tapeli wapo wengi kaka
 
Article nzuri, ila nawe umejipiga risasi mguuni, umeandika article nzuri na kutufanya tukuone kama wa kutupa huo ujumbe zaidi kuhusu kupndokana na "utumwa wa bosi", yaani tukuone "tegemezi" la kutupa ujumbe maridhawa, alafu unataka kututumia tununue kitabu chako kwa sababu "hamna jinsi"!
Nawe ni kama bosi tu.
 
Naona labda utakuwa hujaelewa.
Wewe kupata maarifa yatakayokuwezesha kuondoka kwenye utegemezi wa ajira yako pekee kunawezaje kuwa bosi wako?
Kitabu ni njia ya ziada ya wewe kujifunza, kama unataka kujifunza zaidi. Lakini kama hutaki siyo lazima, kama umeshaelewa na kuweza kuchukua hatua basi uko vizuri.
 
Kama umedhamilia kutusaidia tupe kitabu bure. Maana na ww umetufanya sisi ni waajiriwa so unataka kufikia ndoto zako za kuuza copy 100.kwa wiki
 
Mimi sidhani kama tutafika kwa staili hii.......ya kila mtu kutaka kujiajiri.......maana sasa kila mtu ni mjasilia mali siku hizi na huo ujasiliamali hua haukui hata kidogo
 
Watu wanajua kucheza na akili za watu na wanajua jinsi ya kuzitumia fursa.....bila ya kusahau kusoma alama za nyakati.....

Think big....
 
Unapoajiriwa na wewe una kuwa na ndoto zako pia na ndio maana kunakuwa na kuangalia utapata mshahara kasi gani na malupulupu mengine ili kuona hiyo ajira itatimiza ndoto zako kwa hiyo kwa kauli yako ya kusema mwajiri anaua ndoto za mwajiriwa sio kweli kwenye ajira mnategemeana akupe mshahara utimize ndoto zako na ww umfanyie kazi atimize ndoto zake
 
Naona labda utakuwa hujaelewa.
Wewe kupata maarifa yatakayokuwezesha kuondoka kwenye utegemezi wa ajira yako pekee kunawezaje kuwa bosi wako?
Kitabu ni njia ya ziada ya wewe kujifunza, kama unataka kujifunza zaidi. Lakini kama hutaki siyo lazima, kama umeshaelewa na kuweza kuchukua hatua basi uko vizuri.
Nimependa jibu lako, wee ni mstaarabu! Asante!
 
Kama umedhamilia kutusaidia tupe kitabu bure. Maana na ww umetufanya sisi ni waajiriwa so unataka kufikia ndoto zako za kuuza copy 100.kwa wiki
Hata nikikuba bure, bado hutakisoma.
Nina uzoefu na hili, nimekuwa natoa vitabu bure kila mwezi, kwa miaka mitatu sasa, lakini ni wachache sana wanaosoma.
Hivyo kama una uhakika utakisoma hiki kitabu, na kunipa mrejesho utakapomaliza kukisoma, na ukachukua hatua basi niandikie email kwenye amakirita@gmail.com na nitakutumia bure kabisa.
Karibu sana.
 
Nilichotaka kusema mwajiri na mwajiriwa wanategemeana, hatuwezi wote kuwa waajiri,cha muhimu kila mtu ajue nafasi yake na kutimiza wajibu wake. Mimi niliyewahi kuwa mwajiriwa ni lazima nihakikishe mapungufu niliyoyaona kwa mwajiri wangu hayatakuwepo kwangu kama mtoa ajira. Ili niweze kufikia malengo na ndoto zangu lazima wasaidizi wangu nao waweze kutimiza ndoto zao.

Mkuu maisha ni kuchagua, na unapata kile unachotafufa.
 
Back
Top Bottom