Vitu 8 ambavyo huwezi amini viongozi wakubwa duniani waliviogopa

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
1:Franklin D. Roosevelt: MOTO

fdr.jpg
Huyu ndiye aliyesema "kitu pekee cha kuuogopa ni kuogopa" au kwa kimombo “the only thing we have to fear is fear itself,”. Cha ajabu rais huyu wa marekani aliyeshiriki kuandika historia ya dunia pale alipomfurusha Adolf Hitler alikuwa Muoga wa moto kuliko maelezo. Chanzo ni kumbukumbu mbaya alipokuwa mdogo alishuhudia Shangazi yake akiungua moto baada ya kulipukiwa na taa. Kwa kuogopa moto hata alipokuwa ikulu alilala milango wazi ili ukitokea moto aweze kukimbia, Hii iliwapa kazi ya kupatrol mara kwa mara walinzi wake. Mke wake alipewa kazi ya kutafuta fundi wa kutengeneza vazi maalumu la kumsaidia ikitokea moto ajali ya moto.

2: Genghis Khan: MBWA

1444996151363929-who-was-genghis-khan.jpg

Huyu ni mtawala wa moja ya dola kubwa sana kuwahi kuwepo ulimwenguni, "Mongol empire". Kiongozi katili kabisa aliyetawala kuanzia china,asia na alipigana na kuteka uarabuni hadi ulaya mashariki. Pamoja na yote hayo aliogopa vitu vitatu MAMA YAKE, MKE WAKE NA MBWA. Inasemekana kulikuwa na mbwa huko maeneo ya mongolia wakali kupita maelezo.


3: Kim Jong II : Kupanda ndege
kim-jong-il_r98m.jpg

Huyu ni kiongozi shupavu kabisa aliyetetemesha dunia na marekani kwa mipango yake ya silaa za NYUKLIA kutoka KOREA KASKAZINI. Wakati baba yake alisafiri kwa ndege mara kwa mara kwenda USSR na Ulaya Mashariki, Yeye alichagua kupanda treni iliyojizatiti vilivyo kivita hata alipohitaji kwenda urusi au ulaya mashariki.Aliwahi kupata ajali ya helikopta na kumuacha na kovu usoni. Akiwa anakagua ndege mpya alishuudia moja kilipuka wakati wa majaribio. mtoto wake rais wa sasa hana hiyo kitu lkn.

4:Augustus Caesar: RADI
24f468d0-76b9-456d-8c92-d0304910f3e2.jpg

Huyu ndiye muanzilishi wa ROMAN EMPIRE, akiitawala dunia nzima kwa mkono wa chuma. Hadi leo mabaki ya utawala wake yanaendelea kuwepo.
Amewahi kunusulika kufa kwa radi iliyoishia kumuua mtumwa aliyekuwa karibu yake. Japo alienda kumshukuru mungu wake Jupiter lakni hadi anakufa hiyo kitu ilikuwa anaiogopa kupita maelezo.

5:Heraclius: MAJI
heraclius-by-rossen-toshev-from-rulers-of-the-byzantine-empire-published-by-kibea.jpg

Kiongozi mkubwa na mashuhuri katika historia ya dunia hada Uislamu,Huyu alikuwa kiongozi wa dola ya CHUMA ya Urumi kipindi uislamu unaibuka miaka ya miatano miasita. Aliwahi kuandikiwa Barua na Mtume Mohamad SAW kumshawishi awe muislamu, pia aliamini kuwa Mtume alikuwa mtume wa haki na ilibaki kidogo abadili dini(unaweza kufuatilia). Kiongozi shupavu nguli katika vita aliogopa maji kuliko kawaida. Lakini hii ilichangiwa sana na utabili wa msihiri mmoja aliyemtabilia atakufa kwa maji.

6: Peter THE GREAT: MENDE

peter_the_great_of_russia_detail_1838.jpg
Huyu ni mtawala shupavu kabisa wa urusi ya enzi hizo, Alianzisha mji wa ST petersburg na kuamishia mji mkuu huko badala ya moscow. Aliogoza taifa lililokuwa na nguvu ulaya nzima akitawala hadi maeneo ya scandinavia.Huwez kuzugumzia ukubwa na ushawishi wa russia duniani bila kumtaja mbabe huyu. Lakini alikuwa muoga wa MENDE kulik kawaida.Akigundua nyumba ina mende anahama, Aliwahi kumpiga ngumi askari wake aliyemdanganya nyumba haina mende baadae akaona mende kafa ukutani, kisha akaondoka na troop. alikuwa ameenda kumtembelea kwake huyo askari.

7:Muammar Gadhafi: Maghorofa marefu na Kupanda ndege muda mrefu juu ya maji/bahari

gaddafi-3_1780857b.jpg

Huyu jamaa alikuwa ni mtata sana kufanya nae kazi. Inabidi uwe na akili ya ziada ndio mtaelewana. Alikuwa anaogopa kusafiri juu ya maji muda mrefu zaidi ya masaa nane. Alipohitaji kwenda venezuela au marekani ilibidi wasaidizi wake wabuni route zisizomsababisha asafiri muda mrefu juu ya bahari.Wakti mwingine walitua ureno kwanza badala ya kwenda marekani moja kwa moja. Alikuwa hapendi kabisa kukaa ghorofani. Kila hoteli aliyopangiwa ilikuwa ni floor ya chini, ndio maana alichagua kwenda NEW JEARSEY kwenye makazi ya chini ya kifahari au kuweka Hema tu.

8:ADOLF HITLER: MADAKTARI WA MENO
Kfp9Pmh.jpg

Hitler alikuwa anahudumiwa na daktari wa meno wa kiyahudi.MAtatizo mengi ya kiafya mdomoni aliyapata kutokana na hofu yake juu ya daktari wa Meno. Kitabu kiitwacho "DENTIST OF THE DEVIL" kinamuelezea daktari wake mwingine Blaschke akisema hitler hii kitu ilimsababishia kunuka mdomo, meno ya njano na magonjwa ya fizi. Hii ilimsababishia kudhoofika sana kiafya katika siku za mwisho mwisho wa WWII. Aliwahi kusema ni kheri kubaki na meno mawili kuliko kupitia mikononi mwa hao madaktari. Mnazi mwingine Luftwaffe aliwahi kulia kabisa alipokuwa akitoka kwenye kiti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom