Vitimbwi vya majini na hila zao

Vitimbwi vya majini na hila zao

Joined
Aug 26, 2018
Posts
5
Reaction score
2
A,aleykum warahmatullah wabarakatu naam ndugu zangu na wapenzi wa masomo yangu leo tutaendelea na uchambuzi wetu wa majini na VITIMBWI vyoa na HILA zao ikiwa ni sehemu ya 2 tuanzie hapa

SHWTANI NI NANI?
SHETANI ni ni tabia ya maasi itokanayo na matendo maovu ayafanyayo binadamu ama jinni hivyo kauli hii tunapata kufahamu kwamba hata binadamu anaweza kuwa ni SHETANI

ALLAH katika baadhi ya haya zake amelitaja sana hili jina la SHETANI wanazuoni wa lugha wamekubaliana kwamba ALLAH hapa amemtaja huyo Jinni kwa sifa yake na ifahamike huyo SHETANI WA KIJINI ana majini mengi yenye kuashiria sifa zake ambayo hayo majina alikuwa nayo kabla ya kukufuru kwake

NINI KAZI YA SHETANI NA MALENGO?

Tuwe makini kwasababu tunakwenda hatua kwa hatua tutakuja kuona kwanini leo majini wa kishetani wanawaingia watu wake kwa waume
KAZI YA SHETANI swali hili analijibu ALLAH mwenyewe katika kitabu chake kitukufu
(Shetani ni adui kwenu nanyi mfanyeni adui kwani analiita kundi lake liwe katika watu wa motoni) qur-an35-6
Aya hiyo inatufahamisha shetani ni nani kwetu na kusudio lake nini kwetu sisi watu
Allah anaendelea kutujuza kwamba (Ambae anatia was was katika vifua vya watu) qur-an 114:5 hapa pia tunapata kujulishwa kazi nyingine ya huyo Shetani. Na anatutia was was ili tupate kumuogopa au kumtii ili atukufurishe,

HUTOKANA NA NANI HUYO SHETANI?
Tazama majibu ya Allah hapa katika sura ya 114:6 nini anasema? Anasema (Hutokana na Majini na watu) hapa nadhani tutakuwa tumekubaliana kwamba huyu Shetani hutokana na sisi watu na majini na hakika ndio wapo watu ambao wao wanapenda kuwaona wenzao wakiwa katika hali za kukosa amani hawaoendi kuona watu wanafurahia maisha yao wako teyari kuvunja ndoa za watu. wanafurahi wenzao wakifukuzwa kazi ,wanapenda wao waonekane wanakusaidia wewe wanassma uongo wa kupamba pamba maneno ili uwasujudie Anagalia Allah anatuambia nini katika kitabu chake kisichokuwa na shaka
(Na hakika tumemfanyia kila nabii maadui mashetani wa kijini na kibinadamu wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba pamba ya udanganyifu)qur-an 6:112

Hapa tunajulishwa kwamba hawa mashetni wa kijini na mashetani wa kibinadamu walikuwepo kila zama za kila nabii na kazi yao kubwa ilikuwa ni kusema na kufundishana maneno ya kupamba pamba ya udanganyifu maana yake ni kwamba maneno hayo utakapoyasikia basi wewe utafahamu ni ya ukweli lakini kumbe ni uongo ili wakutie katika kundi lao

Inshaallah katika darsa lijalo tutaangalia mfano wa maneno hayo kisha tutajitathimini je kwa maneno hayo wangapi tumenusurika na wangapi tumeangamia

Kwa maswali zaidi tukutane what-up 0757144465 au piga 0656228832
Nasisitiza mama zangu wajawazito tumieni sana zao la tende kwa kulila litawafanya kuwa na nguvu mpaka katika kipindi cha kujifungua lakini pia mtaepuka kuzaa kwa operesheni kwasababu tende husaidia pia kutanua njia ya uzazi hivyo humfanya mama kujifungua kwa urahisi bila hata kupoteza damu nyingi

Hasanteni nawatakieni usiku mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shetani wa kijini ana majini mengi. Ustadhi bhana
 
Ahsante Ustazi kwa somo lako. Jf naona inaimarika ina kila aina ya watu

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Nitaifuatilia vyema baadaye.
 
A,aleykum warahmatullah wabarakatu ndugu katika imani na ndugu katika Adam Bwana awe nanyi milele amina leo naendelea na darsa hili la vitimbwi vya majini na hila zake ikiwa ni sehemu ya 3

Katika aehemu ya 2 kwa wale ambao wanafuatilia tumeishia sehemu ambayo Allah anatuambia
(Na hakika tumemfanyia kila nabii maadui wa Shetani wa kijini na wakibinadamu wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba ya udanganyifu) qur-an 6:12
Na tukasema kwamba maneno haya ni yale ambayo wewe ukiyasikia utasema ni kweli lakini ndani yake ama msemaji wa hayo maneno hana ukweli anasema ili aaminike apate kukufurisha watu baadae.Tutizame mifano ya maneno hayo

(1)TUNAKULINDA aya ni maneno ambayo majini huyatumia sana wakiwa katika vichwa vya watu.JINN anaweza akapandisha katika mwili wa mgonjwa akasema mimi huyu ndio namlinda nipo nae tangu udogoni lakini ajabu huyo mlinzi yupo ndani ya mwili anasema kwa kupitia kinywa cha mgonwa na mgonjwa anazidi kuteseka kadri siku zinavyokwenda ama kupoteza Mali zake kwa kujitibu kwa waganga mbali mbali kila unapokwenda kwa mganga unaagiziwa mbuzi unapeleka na kupona huponi
Na watu wanaamini wanalindwa na majini sasa tutizame Mwenyezi mungu anatuambia nini kuhusu kuamini ulinzi wa mashetani wa kijini

(Na ambao wamekufuru walinzi wao ni mashetani huwatoa katika nuru na huwaingiza katika kiza hakika watu hao ni watu wa motoni milele)Qur-an 2:257
Wafasirina wanakubaliana kwa pamoja kwamba kiza kilichotajwa hapo ni uchawi na nuru ni ile njia ya kumtegemea ALLAH nadhani naeleweka basi hapa tunagundua kwamba kumbe mashetani au majini hututoa katika njia sahihi na kutupeleka katika batili

(2)HATUTAKI UCHAFU WA KUZINI LAKINI NGOMA KUNYWA DAMU NA POMBE WAKO TEYARI
Majini wa kishetani Mara nyingi sana tena sana huzuia watu wao kuzini yani kufanya tendo la ndoa na mwanamke au mwanaume usiyekuwa na ndoa nae japo kuwa kuna watu wameowana na wenyewe pia wamewekewa masharti na majini namna ya kufanya tendo la ndoa wanafanya kwa siku maalum ambazo wamepangiwa na majini wao.Sasa jini anakukataza kuzini lakini jini huyo huyo akakuamuru umpigie ngoma(Apungwe) achinjiwe mnyama kisha yeye akanywa ile damu kupitia kinywa chako au pombe. Swali la kujiuliza ikiwa majini nadra kuonekana hivi wanashindwaje kwenda machinjioni wakanywa damu pale watakavyo basi tujue lengo lao ni kutukufurisha.Sasa sisi binadamu uwa hatujipi muda wa kujiuliza huyu jini hataki uzinifu lakini mbona damu anataka pombe anataka je uhalali wa damu na pombe uko wapi?

(3)KUJIITA MAJINA MAKUBWA YA UTUKUFU
Sharifu,Ruhani, Walii lakini pia hujifanya wanahimiza ibada.kutaka kusomewa qur-an au wao wenyewe husoma pia na baadae umuingiza mtu katika uganga na kuanza kupiga ramli na kufukuza wachawi pasipo kuwakamata. Wapo watu ambao wanapolala usiku hushtuka na kuanza kupiga kelele mtu huyo uweza hata kutoka nje kana kwamba anapigana na watu huu ni uongo wa majini wa kishetani kutaka kuaminika kwa watu ili malengo ya kukufurisha watu yatimia.MTU Huyo uwa anakuwa na jini kichwani jini anapoulizwa anasema kuna watu wabaya yani wachawi wamekuja wanataka kumdhuru kiti wangu nimewafukuza swali la kujiuliza kwanini asiwakamate kwanini asiwafukuze yeye kama yeye mpaka akae katika mwili wa binadamu ndio awafukuze hao majini.Hivi ni kweli bodigad wa rais amewaona maadui atamuamsha rais ili wote wamkimbize adui yule? Hapa jinni atsema Mimi huyu namkinga na kumuonyesha mambo mengi sana

Inshaallah tutaendelea na darsa hili panapo majaliwa ya Karima nisiwachoshe sana .Nakaribisha maswali katika mtandao wa whatup 0757144465 au call me 0656228832
Darsa la nyota litaendelea pia endeleeni kufuatilia
Mwisho niseme kwa wale wenye matatizo ya mkojo.mkojo unatoka kwa tabu sana basis nenda duka la dawa za kisunna nunua dawa inaitwa Uwatu na Nanaa ukipata nipigie kwa namba zangu nikuelekeze namna ya kuzitumia maelekezo ya dawa natoa bure kabisa
Hassanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A aleykum warahametullah wabarakatu ndugu zangu katika imani na Amani ya bwana iwe nanyi milele kwa wale ndugu zangu katika Adam.Tunaendelea na darsa letu tulipoishia sehemu ya 3 tuliona namna gani ambavyo MAJINI wa kishetani wanavyoweza kusema maneno ya uongo ya kupamba pamba ili waaminike kwa watu na kisha kuwaingiza katika kufuru.Leo tunaendelea na sehemu ya 4

JE KWELI KUNA MAJINI WEMA?
Allah anatupa jibu la swali hili kupitia kitabu chake kitukufu qur-an kareem anasema kumwambia bwana mtume MUHAMAD S.AW
(Taja ewe MUHAMMAD tulipowaleta kwako MAJINI kusikiliza qur-an basi waliobudhuria walisema sikiluzeni na ilipokwisha somwa qur-an walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya)All ahqaaf aya ya 29
Endelea na hiyo sura mpk aya ya 32

Hivyo kwa mujibu wa aya hizo tunaona kwamba wako majini ambao wao walifuata matakwa ya mola wao baada ya kusikia qur-an na wakaenda kuwaonya majini wenzao

Allah s.w.t anaendelea kutueleza kwamba kwa kutunukulia maneno waliyossma majini na akika Allah anajua yale tusiyoyajua anatueleza namna majini walivyosema baada ya kusikia qur-an wale walioiamini walisema(Na katika sisi wamo wema na wengine kinyume na hivyo tumekuwa njia mbali mbali)qur-an 72:11 wakaendelea kusema majini hao
(Na hakika katika sisi wamo waislamu na wamo kati yetu wanaoacha haki basi waliosilimu hao ndio waliofuata uongofu)qur-an72:12

Hivyo basi kazi ya majini hao ni kufanya ibada kama walivyoamrishwa na mola wao/wetu.Majini hawa hawamuingii mwanadamu wala kumuotesha mandoto mabaya au kumtia maradhi. Sasa ikiwa wewe ndugu yangu umekwenda kwa mganga ,mganga huyo akapandisha majini ili akutibu kwa kutumia hayo majini mwambie hapana mwambie na wewe ni mgonjwa kama mimi wote tunatakiwa twende kwa SHEKH akatusomee aya majini yaondoke katika viwili wili vyetu
Na kama wewe unayefuatilia unatibu kwa kutumia majini basi kaa ukijua umeingia katika mtego wa shetani na kashakukufurisha. Hapa nieleweke uganga sio haramu Bali kuna matendo ambayo yakifanyika katika uganga basi uganga huo unakuwa ni haramu mfano
(1)KUPIGA RAMLI AU BAO
(2)KUVAA HIRIZI ukiamini hirizi ile ndio inakulinda au inakuletea Mali.Kuna nchi wanavaa hirizi kama pambo kama vile mwanamama anavyovaa eleni n.k
(3)KUNYWA DAMU,POMBE
(4)KUFUKIA VITU MAKABURINI
(5)KUWAFUKIA WANYAMA WAKIWA HAI.WENGINE UWASHONA MIDOMO WANYAMA HAWA KISHA HUWAFUKIA
(6)KUKATA VIUNGO VYA BINADAMU MWENZAKO AKIWA HAI AU MAITI

Hayo ni baadhi ya mambo yanapofanyika katika tiba yako basi umeingia katika ushirikina na hata kama utafanikiwa Yale uliyoyaendea basi kaa ukijua umejitibu kwa ushirikina na una kesi ya kujibu mbele za mola wako

Jamani darsa ni ndefu tuishie hapa kwa Leo nakaribisha maswali yenu katika mtandai wangu wa whatup 0757144465au call me0656228832
Njpo katika ziara ZANZIBAR nikiwa nimemaluza pale Ubago,Kitumba,Machui, Ndagaa na sasa naelekea Ndigani na huku ofisi yangu inapatikana KIDIMNI KWA KANDURU nakukaribisheni nyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom