Ole Shider
Member
- Oct 17, 2014
- 16
- 15
Ni takribani siku nane sasa toka Katibu Mkuu wa CCM Ndgu Abdulrahaman Kinana aanze ziara yake Mkoani Arusha..
WanaCCM wote wanatambua na kuthamini jitihada anazofanya Kinana katika kuhakikisha kuwa Chama chao kinarudi katika misingi yake kutokana na ziara zake alizozifanya yapata Nchi nzima.
Ziara hii ya Kinana Mkoani Arusha imeibua mambo mengi sana hasa kwa wale wanaotajwa kuutaka Ubunge wa UWT Mkoani Arusha nafasi inayoshikiliwa na Namelock Sokoine kwa sasa.
Wanaotajwa kuonekana kutamani na kuanza kuvizia nafasi hiyo ni pamoja na Catherine Magige, na Clementina Mollel ambao wote wameonekana katika ziara ya Kinana toka siku ya kwanza na yawezekana mpaka ya mwisho.
Vikundi mbali mbali vimeonekana vikisimama kando na kuulizana maswali mengi wengi wao wakiwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha.
Hoja ya msingi wengi wameshangazwa na kujiuliza mtu kama Catherine ambaye kwanza alipaswa kuwa Bungeni inakuwaje hajaenda mpaka leo? Lakini pili hii nafasi ya UWT bado ina Mbunge aliyepo na katika ziara zake Katibu Mkuu wa CCM yeye amekuwa akisisitiza kuwa Wabunge wa CCM walioko madarakani wasisumbuliwe na waachwe wafanye kazi zao. Lakini la tatu watu wanashangazwa Catherine ni nani hata aweze kuwa kwenye msafara toka siku ya kwanza??
Baadhi ya wapambe walioko karibu na Catherine wakiongozwa na kijana aliyejulikana kwa jina moja la Amo na fatuma Ngairo (Katibu wa Vijana Wilaya ya Arumeru) ambaye alidiriki kumshambulia kwa matusi mmoja wa anayedaiwa kutaka kugombea Ubunge wakati wa Mkutano Wilayani Arumeru alisikika akielezea watu kuwa Catherine ameshaahidiwa Ubunge na Nape Nnauye pamoja na Katibu Mkuu....
Mpashaji huyu alieleza kuwa hata walipokuwa Longido Katibu Mkuu aliita baadhi ya Watendaji wa jumuiya na kuwapa maelekezo wamsaidie Catherine kutokana na imani yao kuwa moja. Katibu huyu vile vile ameonekana kulaumiwa sana na viongozi wa Wilaya ya Arumeru kwa kuacha ofisi kwa takribani siku 9 na kwenda kwenye ziara ya katibu Mkuu jambo ambalo lilipelekea Jumuiya ya Vijana kutoonekana vyema katika mapokezi ya Katibu Mkuu. Kinachoonekana sasa ni kwamba yeye ameamua kuwa Katibu wa Mbunge na si wa Jumuiya...
Baadhi ya waandishi wa habari walipata wasaa wa kuzungumza na Clementina Mollel ambaye inasemekana alishambuliwa kwa matusi na Ngairo. Clementina alikiri kuwa alidhalilishwa sana "huyu binti mimi kanishangaza sana kwanza umri hatulingani na hakuna kokote kule ambako mimi na Fatuma tunakutana ila kanidhalilisha sana na niweke sawa tu hata kama ni Ubunge hivi kweli tutaupata kwa namna hii?? Manake naamini bado watajitokeza wengi sasa kama hivyo ndivyo tutatukana wote?? Mi nadhani hii si CCM tunayoijua hatupaswi kufika huku ila hili nitalipeleka kwenye mikono ya sheria manake huyu binti kanitamkia wazi kuwa atanionesha" alinukuliwa Clementina akizungumza kwa hasira.......
Catherine alipopigiwa ili kuulizwa tuhuna za kubebwa na Nape pamoja na vikao vya Longido na tuhuma za kutuma wapambe wake kutukana wabaCCM wenzie na tuhuma nyingine ya kutaka kumshughulikia Katibu wa Vijana wa Mkoa eti kwa kuwa hamuungi Mkono simu yake iliita bila majibu...
Hata hivyo baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Arusha wameapa kula sahani moja na Catherine manake hana uungwana hata kidogo na dharau zake zitamgharimu...... "Unajua huyu binti bana huwa anajifanya kujitoa ufahamu sasa leo kwa kuwa ana hitaji lake kajifanya kurudi kwa kasi ila kitaeleweka tu manake yeye anajifanya ana wakubwa sasa sisi tulio na wadogo tutajitahidi " alinukuliwa mwandishi mmoja wa gazeti la kila siku na mwandishi mwingine anayeiwakilisha radio moja Mkoani Arusha.....
Mwenyekiti wa UWT Mkoa alipoulizwa kama anajua haya yanayoendelea Mkoani kwake alisema kwa ufupi "Mbunge niliye naye sasa hivi ni Namelock Sokoine na kama kuna vikao vinavyoendelea mimi sivijui ila kama watu wamefikia hatua ya kuanza kutukanana na kulumbana nadhani wamefika mbali........ Muda ukifika taratibu za Chama zitafuata Mkondo wake....... nataka niwahakikishie hatutachagua mtu kwa imani yake wala dini wala kabila lake mwanamke yeyote anayekubalika na mchapa kazi tutakwenda" Mwisho wa kumnukuu.
Aliulizwa vile vile Mwenyekiti wa Vijana kama kapata habari kuhusu Katibu wake kushughulikiwa....... "Eeeeh jamani tena? Haya mambo kwa kweli ni shidaa lakini binafsi Sijasikia hizo habari ila hivi Kwani Mwajuma na UWT wapi na wapi... Halafu labda niwasaidie Mwajuma anahamishwa kwa utaratibu aliyemleta ndiye atakaye mwamisha.... Halafu mnisaidie hili Jumuiya ya Vijana hapa Mkoani Arusha imetulia na Sadiffa nimemweleza hilo embu tuachwe tukitumikie Chama sasa tuna mengi mwaka huu sana......... Mwajuma hakuja hapa kwa ajili ya kuandaa Wabunge wa UWT au wa Vijana na hata mimi binafsi nikisikia anafanya kazi hiyo ataondoka tu afanye kazi ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana na Chama period! Vijana wetu huku wana matatizo mengi sana bana...Tunaweza kuonekana watu wa hovyo kila siku nyie mnataka kuhamisha watu hili haliwezekani na wala halikubaliki......."
Alipoulizwa kuhusu Katibu wa wilaya kuacha ofisi Mwenyekiti alisema hilo halajipata ila litakapokuja kwa utaratibu watalifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu zilizopo ndani ya Chama....
Ziara ya Kinana inaendelea Mkoani Arusha ambako anatazamia kumaliza tarehe 21 kwa kuhitimisha kwa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Sheikh Amri Abed ambapo baada ya hapo ataelekea Kilimanjaro......