Vitabu vipya vya taasisi vinaokoa au vinazamisha elimu ya Tanzania?

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
765
Nahisi hatujajua thamani ya elimu. Tumezoea kusikia kwenye soka Tanzania ikiitwa “kichwa cha mwendawazimu.” Nahisi kama kwenye Elimu nako hakuna tofauti.

Lakini nisiseme sana, labda teleskopu yangu ina ukungu. Mniwie radhi kama nitakuwa nimekosea. Nina tu-swali tuchache naomba mchango wa mawazo.

Endapo nitakuwa sahihi kama ninavyohisi, basi, “Somo hilo hapo juu lahusika!”

Vyombo vya elimu vilisema kuwa kuwapo kwa vitabu mashuleni toka kwa wachipishaji wengi (viliitwa ‘utitiri wa vitabu’) ni tatizo --- JAPO MTU ATAJIULIZA, UNAEPITISHA VITABU SI NI WEWE? KWA NINI USITEUE KIMOJA KWA KILA SOMO UNACHOONA KIMEKIDHI VIGEZO ULIVYOWEKA WEWE MWENYEWE?

Basi, suluhisho likatangazwa kuwa ni Taasisi ya Elimu (TIE) ndiyo inatakiwa kuandika hicho kitabu kimoja kwa kila somo kwa ajili YA NCHI na “future” yake.

Mantiki ya tamko hilo ni kuwa: TIE ndio WENYE UWEZO wa kuandika vitabu (na sio “Makanjanja” – yaani waandishi binafsi kama walivyoitwa wakati ule).

Sasa naomba nizungumzie kitabu ambacho sasa ndio kimeandaliwa na TIE chenye jina: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, kisha wadau tusaidiane kubainisha iwapo hiki: (a) kinatimiza malengo yale (b) kinafaa kutumiwa na watoto wetu (c) kinabeba hatma tarajiwa ya Tanzania.

Haya ni MACHACHE kati ya mengi niliyoyabaini kwenye kitabu hiki:

1. Uk 3 wameandika: “Tusimulie matendo tunachofanya tunapoamka. ---------- tunachofanya??
upload_2017-5-10_12-15-54.png
2. Uk 6 swali la 1: Taja majina yawanyama hawa. ---- “yawanyama” ni neno moja??
upload_2017-5-10_12-16-12.png
3. Uk 10 swali la 2: Ni jina la picha ipi lenye sauti ya mwanzo isiyofanana na sauti ya mwanzo ya jina la picha nyingine? --------- Hivi hii ni sentensi ya mtoto wa Darasa la 1? Imerudiwa mara nyingi kwenye kurasa mbalimbali.
upload_2017-5-10_12-16-29.png
4. Uk 26: “tamka za herufi” ni Kiswahili sahihi? Neno “Silabi” --- Haya ndiyo matumizi ya herufi kubwa? Swali la 5, neno “bima” kwa mtoto wa Darasa la 1? Akiuliza, "Bima ndio nini mwalimu?" mwalimu atajibuje hadi aelewe?
upload_2017-5-10_12-17-1.png
5. Uk 37 swali la 9 linasema: Tazama picha zifuatazo kisha kamilisha sentensi hizo. ---- “sentensi hizo”????
upload_2017-5-10_12-17-16.png
6. Uk 39 swali la 3 linasema: Soma habari hii kisha jibu maswali yafuatayo: ------- Hivi unaweza kutumia neno “yafuatayo” kwa mtindo hii? Sentensi mwisho wa habari inasema: “Bei ni mia.” ---- duh!!!!!
upload_2017-5-10_12-17-31.png
7. Uk 67 swali la 2 linasema: Keki na pilau ni nini? ----- Hivi unaweza kuuliza hivi ili mtoto aseme “ni tamu”? (maana ndilo jibu wanalotaka)
upload_2017-5-10_12-17-51.png
8. Uk 117 swali la 7 linasema: Baba yake ina nguvu. -------- Are we serious? Hata Wakenya nadhani hawaandiki hivi.
upload_2017-5-10_12-18-19.png
9. Uk 119 swali la 2 kumeandikwa: “Unda na tusome silabi …” -------- Sijui wewe msomaji unaonaje hapo?
upload_2017-5-10_12-19-30.png
10. Uk 125 kuna embe imekatwa nusu halafu imeitwa “kokwa”
upload_2017-5-10_12-20-1.png
11. Uk 127 kwenye habari kuna sentensi inasema: Mimi ni zaidi yako, bila mimi huwezi kwenda nchi za mbali.-------- Hii ni sentensi moja kweli?
upload_2017-5-10_12-20-23.png
12. Uk 128 swali la 10: Soma habari hii. Kisha jibu maswali. ---------- Hizi ni sentensi mbili kweli? Sentensi mbili za mwisho zinasema: Mwalimu Limo alimwambia Furaha asikate tamaa. Aendelee kusoma kwa bidii atafaulu. ---------- Ndugu msomaji, wewe unazionaje ladha yake?
upload_2017-5-10_12-20-44.png
13. Jambo la mwisho kwa hapa, angalau mojawapo kwa upande wa usanifu, ni kuwa: unaonaje ukisoma kitabu ambacho kimejaa BOLD, BOLD, BOLD letters kila sehemu? Je, huo ni uandishi mwafaka kweli?

Sasa, kitabu chote kiko kimtindo huu.

……………….

Kama nilivyosema, “HAYA NI MACHACHE TU.”

Please, somebody do something about our education!

Maoni yangu:

1. Serikali waendelee kusimamia ubora wa vitabu kupitia EMAC.

2. Kama TIE wanaandika, nao washindane na wachapishaji wengine kwa usawa lakini sio kupitisha sheria ya kufungia wengine, kisha wanaleta vitu kama hivi - vinginevyo basi waboreshe kwelikweli.

3. Kama vitabu vingi ni utitiri na ni tatizo, basi chagua kimoja KILICHO BORA kwa kila somo toka kwa mchapishaji YEYOTE – kwa mujibu wa vigezo unavyotaka mwenyewe – ambavyo sina uhakika kama kipimo cha vigezo hivyo ni vitabu hivi vinavyoandikwa na TIE kwa sasa.

4. TIE wanawezaje kuwa waandishi na hapohapo ndio mahakimu wa kuhukumu kazi za wachapishaji wengine? (kwa maana kwamba EMAC imekuwa ni sehemu ya TIE)? Je, watatenda haki kwa watu ambao hawangependa wawazidi? Je, wao wanahakikiwa na nani? BAKITA wanawahikiki? EMAC gani inawahakiki wao?


Ni hayo tu Watanzania wenzangu.
 
nimejaribu kujiridhishda haya mapungufu uliyo yaainisha, ni kweli nimeyabaini. hongera sana kwa kuwa mfuatiliaji makini. lakini nitatofautiana na wewe kuhusu pendekezo la kurudi kwenye soko huria na kisha kumwachia EMAC jukumu la kukagua na kuthibiti ubora wa vitabu nchini. nina vitabu vingi vilivyo idhinishwa na EMAC vinamapungufu pia. nadhani TETwanatakiwa kuongeza umakini zaidi ktk kuandaa vitabu. makosa uliyoainisha yaliyo mengi ni ya kiuandishi (typing errors). lkn pia serikal haijazuia kutumia vitabu vingine kwa rejea.
 
nimejaribu kujiridhishda haya mapungufu uliyo yaainisha, ni kweli nimeyabaini. hongera sana kwa kuwa mfuatiliaji makini. lakini nitatofautiana na wewe kuhusu pendekezo la kurudi kwenye soko huria na kisha kumwachia EMAC jukumu la kukagua na kuthibiti ubora wa vitabu nchini. nina vitabu vingi vilivyo idhinishwa na EMAC vinamapungufu pia. nadhani TETwanatakiwa kuongeza umakini zaidi ktk kuandaa vitabu. makosa uliyoainisha yaliyo mengi ni ya kiuandishi (typing errors). lkn pia serikal haijazuia kutumia vitabu vingine kwa rejea.
Asante sir longo kwa response. Hapa wala hatugombani. Ni kweli kuna vitabu vingi vya EMAC vyenye upungufu. Lakini kama hawakuweza kudhibitiwa kipindi kile, basi hata sasa haitawezekana. Na kama sasa inawezekana, basi hata zamani ingewezakana. Kwa hiyo, kumbe basi suluhisho lingekuwa kuimarisha huo udhibiti na sio kusema ni TIE pekee ndio wanaruhusiwa kuandika vitabu vya Kiada. Pili, makosa yaliyomo yasiyo ya kiunandishi ni mengi pia. Lakini pia, huo si utetezi wa kupeleka vitabu shuleni vyenye makosa haya na kujitetea kuwa eti afterall ni typing error tu. Na kama kitabu kidogo tu hiki chenye font kubwa hivi kina makosa, je, kitabu cha sekondari kikubwa na chenye font ndogo? Mwisho, nakubaliana nawe kuwa kama TET wana UWEZO wa ufanya kazi bora, wala hakuna tatizo.
 
Back
Top Bottom