Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,525
- 22,465
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi maalum au special forces wakiwa wanamshikilia mmoja wa magaidi wa ISIS: Picha na AFP
Majeshi ya Iraq yameingia ndani ya eneo la magaidi wa kikundi cha magaidi cha ISIS wakijaribu kuwaondoa magaidi hao ndani ya mji wa Mosul ambao umekuwa ngome yao kuu tangia mwaka 2014.
Majeshi hayo ya Iraq yakiongozwa na vikosi maalum vya jeshi shirikishi la nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani na baadhi ya nchi za kiarabu, wamekwishakomboa uwanja wa ndege wa Mosul na sasa wanakabiliana na magaidi hao wakipita kufanya msako wa nyumba nyumba hadi nyumba.
Pia majeshi hayo ya Iraq tayari wamekomboa bwawa la kuzalisha umeme wa Mosul au Mosul dam.
Wakazi wengi wa mji wa Mosul wamelazimika kuuhama mji huo ambao ulitekwa na wanamgambo wa ISIS mwaka 2014 baada ya kuuawa kwa kiongozi wao Abu Abdulrahman al-Bilawi.
Licha ya kuuteka mji huo magaidi hao wa ISIS waliteka sehemu muhimu za kimkakati wa kiuchumi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Mosul na pia bwawa la kufua na uzalishaji umeme ambalo lilikuwa ni tegemeo kwa wakazi wapatao milioni moja katika bonde la mto Tigris.
Miongoni mwa majeshi shirikishi ni wanajeshi wa Peshmerger ambao ni wa kabila la wakurdi na wenye majukumu ya kuhakikisha wanasafisha njia kwa majeshi ya ardhini ya Iraq yapatayo 100,000, huku wakisaidiwa na Marekani ambayo inatumia ndege za kivita kutupa makombora kutokea angani.
Mwezi October mwaka jana waziri mkuu wa Iraq bwana Haider al-Abadi alitangaza rasmi kuanza kwa operesheni hiyo ambayo imeendelea mpaka leo ambapo vita inaelekea ukingoni..
Wakazi wa Mosul wakiwa njiani kupisha mapambano kati ya majeshi ya Iraq na magaidi wa ISIS: Picha na AFP.
Habari zaidi kuendelea kukujia.