Vita vya Siku 33 kati ya Israel na Hizbollah

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,450
2,757
Kikosi cha jeshi cha Hizbollah ni kikosi cha waislamu wa dhehebu la Shia ithna asharia kinachopata mafunzo na udhamini kutoka kwa jamhuri ya kiislamu ya Iran. Ikifika tarehe 14 Agosti 2016, imetimia miaka kumi tokea vilipohitimishwa vita vya siku 33 ambavyo vilianzishwa na utawala wa Israel dhidi ya ardhi ya Lebanon mwaka 2006.

Majeshi ya utawala wa Israel tarehe 13 Julai 2006 yalianza kuishambulia ardhi ya Lebanon, ingawa utawala huo ulishindwa kufikia hata lengo moja kwenye mashambulizi hayo. Mapigano kati ya majeshi ya Israel na wanamapambano wa Hizbullah yalihitimishwa baada ya kutolewa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 14 Agosti 2006.

Licha ya kutolewa azimio hilo, utawala huo uliendelea kufanya uchokozi wa mara kwa mara dhidi ya ardhi ya Lebanon. Serikali ya Lebanon mara kadhaa imefikisha mashtaka yake kwa Umoja wa Mataifa kutokana na chokochoko zinazofanywa na Wazayuni, lakini umoja huo haujachukua hatua zozote za kivitendo za kukomesha uchokozi na mashambulio ya majeshi ya Israel.

Imeripotiwa kuwa, katika vita hivyo vya siku 33 dhidi ya Lebanon, wanajeshi 119 wa jeshi la Israel waliangamizwa na mamia ya wengine walijeruhiwa. Vita hivyo pia vilisababisha raia 1,200 wa Lebanon wengi wao wakiwa wanawake na watoto kuuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la al Akhbar lililochapishwa leo mjini Beirut, Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel juu ya kuendeleza jinai na ukaliaji wake wa mabavu wa maeneo ya Waarabu.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, wanamapambano wa Hizbullah wako makini kukabiliana na utawala wa Israel na kusisitiza kwamba, katika siku zijazo hakutakuwa na mstari mwekundu katika vita na Wazayuni maghasibu.

Aidha Katibu Mkuu wa Hizbullah ameendelea kueleza kwamba, kuwepo kwa muqawama nchini Syria hakuathiri maandalizi ya Hizbullah ya kukabiliana na majeshi ya Israel na kusisitiza kwamba ‘kama vile tulivyoweza kulinda kikamilifu mipaka ya kusini mwa Lebanon, tutaendelea kulinda mipaka yetu na Syria’. Sayyid Hassan Nasrullah amezungumzia vita vya hivi karibuni huko Ghaza na kubainisha kwamba, wana wa Palestina wana haki ya kupambana na utawala hadi watakapopata ushindi kamili.

Ameongeza kuwa, vita kati ya wanamapambano wa Palestina dhidi ya majeshi ya Israel vimeimarisha zaidi uhusiano wa Hizbullah na Hamas.israel ndio taifa lenye rekodi ya juu ya uchokozi na uiukaji wa haki za binadamu na kuvunja kanuni za kimataifa kwa kutegemea utetezi inaoupata kutoka kwa serikali ya Marekani.

Israel ilikomesha uchokozi wake kwa nchi ya Lebanon baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanajeshi wa Hizbollah, ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Israel, kipigo hicho kilipelekea majeshi ya Israel kunyoosha mikono na kuomba sulhu katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006.

Najaribu kujiuliza zile s-300 zikitumika kwa sasa israeli itaweza ku stand dhidi ya Iran kama walishindwa na wana mgambo seriously ni vita gani israel ilipigana yenyewe man alone ikashinda embu niwasilishe.
 
Mkuu umeandika kishabiki sana kati ya hao 1200 waliokufa, Hezbollah walipoteza 500 ila Israel haikutegemea upinzan walioukuta walisema wali fail logistically
 
Me naamini km Israel wangeshindwa lazima Hizbbollah wangerudisha milima ya golan iliyotekwa katika vita ya 1967 kwaani ni sehemu nyeti ktk medani za kivita.
 
Mtoa mada kuna kundi la muhimu umekosa kulijumuisha katika mapambano na Israel, kuna kundi ambalo lazima rais wa Lebanon hatokee uko dhehebu moja la wakristo kama sikosei linaitwa Moro, miongoni mwa kundi linarounda HIZBULLAH walitoa mchango mkubwa sana kupambana na Israel katika hivyo vita. unapuzungumzia hivyo vita ilo kundi uwezi kuliacha
 
lengo point yako ni S-300 ya iran vs israel ilo la hizbollah ni nakshi tu,ila kiukweli hawa jamaa israel ni wakorofi si kidogo,ile safari ya kutoka utumwani misri walikuwa wakaidi sana mbele ya mungu"
kwa hali halisi inaonesha awa israel ni wakorofi na wakaidi,
kama walikuwa wakaidi mbele ya mungu sidhani kama wataweza kuzuilika/kupigwa kirahisi
 
Back
Top Bottom