Vita ni uchafu mtupu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,050
Reaction score
61,376
Kipindi vita inachezwa tulio mbali na uwanja wa mapambano tunadhani labda kuanzia asubuhi kazi ya wanajeshi ni kupigana tu risasi. Behind the scene ni mengi yanaendelea vita ni uchafu watu wanauana, posho zinaendelea kutembea, watu wanatajirika. NI mwendo wa ku sign tu madokezo, wanajeshi wanapata utajiri, wengine wameingia vitani maskini wanaenda kuotea zali vitani, wanaiba madini, mahela mtu anatoka vitani tajiri vibaya mno.

Sio tu utajiri uwanja wa mapambano bali Nyuma zaidi viongozi wa kisiasa wanapanga vikao vya usuluhishi kwenye mahotel makubwa wanapata maposho ya maana, kampuni za silaha nako zinaendelea kufanya marketing kukutana na viongozi wa jeshi kufanya madeal ni mwendo wa 10% tu.

Vita ni uchafu, vita ni biashara.
 
Vita ni zoezi la kufanya usafi,unatoa kibaya unaacha unachokitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…