Vita hii ni ya Watanzania wote...

Vita hii ni ya Watanzania wote...

David Djumbe

Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
42
Reaction score
36
View attachment 120190

Mauaji ya tembo katika hifadhi zetu nchini ni janga la kitaifa kwa sasa, nchi inapaswa kuchukua hatua kali na makini kuhakikisha tunakomesha matendo haya ya kikatili yanayohujumu rasilimali za nchi yetu na urithi wetu.
Tembo zaidi ya 30 wanauawa kila siku, hivyo kufanya takribani tembo 1000 kwa mwezi, hali hii ikiachwa ikaendelea kwa muda wa miaka isiyozidi 10 hatutakuwa na mnyama anayeitwa tembo nchi hii.

Vita hii dhidi ya ujangili ni kubwa na ina mtandao mkubwa nchini hadi nje ya nchi, hivyo haiwezi kuwa rahisi kushinda kama Watanzania wote hatutaweza kuunganisha nguvu zetu kupambana na ujangili huu unaoelekea kuangamiza kabisa kizazi cha tembo nchini.

Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutambua athari za vitendo hivi na kila mmoja kutambua wajibu wake katika kulinda rasilimali zetu, tusikubali kuona watu wachache wakiharibu na kuiba utajiri wa nchi yetu huku tukiwatazama tu, ni lazima tujenge uzalendo na tuwe pamoja katika suala zima la kulinda rasilimali za nchi yetu na urithi wetu.

Serikali lazima sasa iweke nia dhahiri ya kupambana na ujangili nchini ,badala ya kulichukulia suala hili kisiasa na kulifanya la majukwaani, nia ya dhati ya kutokomeza biashara hii lazima ionekane kwa vitendo na wale wote wanaokamatwa au kuhusishwa na biashara hii wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Mimi naamini kabisa kama watu wachache wa mwanzo wanaokamatwa wakachukuliwa hatua kali, basi wengine wote wanaojihusisha na biashara hii wataacha wenyewe.

Nawatakia uwajibikaji mwema katika kulilinda Taifa Letu
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwakweli mimi mkuu hamna kitu knachooniuma katika mali za Tz kama mauaji ya rasilimali hizi, wenzetu Africa Magharibi wame-declare faru weusi (black rhino) week iliyopita ndo wamekuwa extinct.

Nafikiria uakaribu wa Wachina na nchi yetu hawa watu hawana huruma taifa lolote duniani ni hatari zaidi hata ya Wamarekani pale wanapotaka kuipata rasilimali fulani. Mfano Zimbabwe wameua tembo wengi sana kwa kupaka cyanide udongo ambao tembo hupenda kuulamba.

Lakini wenzetu South Africa wameanzisha campaign maalum ya "Poachers will be poached"

Inaumiza nahisi mjukuu wangu hawezi tena kumuona tembo na sina hata fedha za kumpeleka zoo za nje kumuona tembo achilia wanyama wengine.

VIP

Ninashawashika kwa Waafrika wanaoishi nchini China na wanaotoka nchi zenye hifadhi ambazo kuna tembo wengi waandamane mpaka kweny ofisi za kiongozi wa China kumfikishia ujumbe wa kudhibiti biashara hii nchini kwake. Wachina wanatia maudhi sana.
 
Cc Chabruma!!!!!!!

Come see the log is getting dry and dry as time goes by!!!!!!!

Waaambieni watoe kero tu mitandao itakuwa calmer place for them to refresh!!!!
 
Back
Top Bottom