Siyo siri mheshimiwa kuwa hali ya nchi inavyokwenda kwa sasa katu hali si shwari. Siyo siri kuwa kuna idadi kubwa ya wananchi ambao hawaafikiani tena au hata kufurahishwa na mambo yanavyokwenda. Haihitaji kuwa umesimama upande upi wa itikadi kuweza kuyaona haya ninayo yasema. Kwa ufupi angalia:
1. Mwelekeo wa kamata kamata za waheshimiwa tuliowachagua kama wewe zinazokoelemea
2. Mwelekeo wa funga funga za waheshimiwa tuliowachagua zinakoelekemea
3. Matamko tata ya walioko madarakani yanakoelemea
4. Nk nk
Katika hali kama hizi hata sasa tunaposikia waheshimiwa kama kina Mbowe wametajwa kwenye vita vya madawa ya kulevya kunakuwa na mashaka kwani katika siasa hizi za Afrika, labda hata Museveni angependa sana kusikia hata kama si kweli kuwa wapinzani wake kama kina Besigye wamehusishwa na tuhuma nzito kama hizi ili watoweke. Labda ni vivyo hivyo kwa akina Uhuru Kenyata na kina Raila Odinga na hata Jammeh na mwenziwe?
Siyo siri mheshimiwa hapa tulipo sasa hivi si pa afya hata kidogo na bila shaka tuendako kama hali hizi za kuendekeza chuki zisizokuwa na msingi zitaachwa kuendelea tuendako kunaweza kuwa kweusi zaidi badala ya kuwa ni kwenye Tanzania ya Viwanda ambazo kampeni zako zilikuwa zimetupa matumaini.
Siyo siri kuwa Tanzania tulikuwa na historia tofauti sana ya kuvumiliana ambayo ili tutofautisha kabisa sisi na mataifa mengine ya Afrika. Mheshimiwa pamoja na nia yako nzuri uliyo nayo kwa taifa hili kwa mwendo tunaoenda nao kufika tuendako ni mashaka makubwa. Historia za mataifa mengi ya Afrika tunazijua. Katika siasa hizi za Afrika zisizokuwa na kuvumilia mawazo tofauti tutakuwa tunajidanganya kama ndimo Tanzania ya viwanda itaibuka. Tumekuwa tukijitanabainisha kuwa sisi ni kisiwa cha amani kimsingi kutokana na kuwa tulikuwa mambo ya msingi ya kuendesha nchi kwa kuzingaia misingi imara ya katiba yetu ambapo uhuru wa maoni ulikuwa suala la kuzingatiwa.
Ushauri wa bure kwako mheshimiwa: Kabla mambo hayajaharibika mheshimiwa itisha Pooooo! Sote kuanzia wewe mheshimiwa turejee kwenye misingi ya Katiba na sheria kwani hapa tulipo siyo siri tume ghafirika na tuendako kuna giza nene. Hatuna sababu ya kuwekeana mazingira magumu yasiyo na sababu ya kuishi katika nchi hii yetu ambayo sote tuliachiwa na mababu zetu ambako hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine.
Ku Retreat siyo ku surrender mheshimiwa. Tutafute muafaka na maridhiano sisi wote kama Watanzania. Sote kwa pamoja hatuwezi kushindwa kufika mahali tukakubali kutofautiana ama kukubali kuafikiana kwa nguvu za hoja zetu. Tujitathimini wapi tumeteleza kwani kuteleza si kuanguka.
Leo hii tuko kwenye kutajana nani anafanya madawa ya kulevya. Mheshimiwa utakumbuka mheshimiwa Mwinyi aliwahi kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani kwenye sekeseke lililopelekea vifo kwenye kuwalazimisha waliotuhumiwa uchawi (kwenye mikoa ya kwenu huko usukumani) kuwataja wachawi wenzao.
Hivi tumesikia anatajwa bwana Makonda kuwa naye huenda anaweza kuwa anahusika na hii biashara. Kwa mwendelezo wa utaratibu huu haitashangaza akitokea mwendawazimu akakutaja wewe mheshimiwa ya kuwa nawe ni gwiji haswaa kwenye hii biashara.
Kwani ni kweli kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na uimara wao vimeshindwa kufanya uchunguzi wao hadi kutegemea kupata taarifa za hawa magwiji tokea kwa waathirika wa madawa haya?