Virusi vya HIV vyaanza kujenga kinga

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714

Virusi vya ugonjwa wa ukimwi vinaendelea kujenga kinga dhidi ya dawa za ugonjwa huo zinazotumika kukinga na kukabiliana na ugonjwa huo,utafiti umesema.

Virusi vya HIV vimeanza kuwa na kinga dhidi ya dawa ya Tenovir katika asilimia 60 ya visa vyote miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika kulingana na utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 1998 na 2015.

Utafiti huo ,ulioongozwa na chuo kikuu cha London,uliwashirikisha takriban watu 2000 walio na virusi hivyo duniani.

Kiongozi wa utafiti huo Daktari Ravi Gupta amesema kuwa matokeo yake yalizua wasiwasi mkubwa.

Kazi hiyo iliochukua miaka minne kukamilisha.Ilianza mwaka 2012 na iliwalinganisha wagonjwa wa ugonjwa huo barani Afrika na wale wanaoishi barani Ulaya.

Huku wagonjwa hao wakigawanywa katika makundi mawili,utafiti huo ulibaini kwamba barani Afrika asilimia 60 ya wagonjwa walikuwa hawatibiki na dawa ya Tenovir huku barani Ulaya idadi hiyo ikipungua na kuwa asilimia 20.

Matokeo hayo ambayo yamechapishwa katika jarida la Lancet kuhusu magonjwa ya maambukizi,ulisema kuwa usimamizi m'baya wa dawa hizo kama vile kutozitumia zinavyohitajika na katika viwango vilivyo sawa huenda ndio sababu ya tatizo hilo.

''Iwapo viwango sawa vya dawa hiyo havitatumika ,virusi vinaweza kukabili dawa hiyo na kuwa na kinga'',Daktari Gupta aliiambia BBC.

''Tenovir ni dawa muhimu katika vita dhidi ya virusi vya ukimwi,kwa hivyo inatia wasiwasi sana kuona viwango vya virusi vilivyo na kinga dhidi ya dawa hiyo'',aliongezea.

Utafiti huo pia umesema kuwa virusi vilivyo na kinga dhidi ya Tenovir vinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.

Chanzo: BBC
 
Duuu dawa ya ukimwi sijui itapatikana lini? Mmh nimemkumbuka babu wa loliondo jamani..
 
King'amuzi cha continental decoder? Virusi vya HIV.
Kweli elimu, elimu, elimu
 
Drug resistance, mbaya sana hiyo kitu.

Scientists wanahitajika kurudi tena field upya, we dont dont know how long will it take to innovate a new drug....
 
Eti Deception kwani kuna ugonjwa unaitwa UKIMWI ????

Hakuna ugonjwa unaoitwa ukimwi.Vitabu vya dini vinasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa",pia,"elimu ni nguvu ya kila kitu".

Hawa jamaa walioleta huu uzushi wametumia akili nyingi sana kutudanganya kiasi kwamba mtu wa kawaida ambaye ni mvivu wa kufikiri ni rahisi kudanganyika.Wametumia dini,vyombo vya habari,movies/sinema,makongamano,matembezi ya maadhimisho ya ulimwi na mambo mengine mengi kurubuni akili za walio wengi kwamba HIV anasababisha ukimwi.

Akili waliyoitumia ni kubwa sana kiasi cha kufanya bongo za watu wengi kukimbilia kupinga bila kuhoji pale unapowaambia kwamba HIV ni nonsense na ukimwi hausababishwi na huyo HIV hewa,pia ukimwi si kitu cha kutisha kama tulivyorubuniwa akili zetu.

Watu wanashabikia upuuzi bila kujijua,siwalaumu kwa hili,bali nawalaumu kwa kutokutaka kujua/kuhoji pale wanaposikia taarifa mpya/tofauti na zile walifundishwa tangu wako na umri mdogo kuhusu suala hili.Ubongo wa watu uko stagnant/umelala na una ganzi kiasi cha kushindwa kabisa kuhoji pale wanapoona au kusikia mikanganyiko inayojitokeza kila siku kwenye jamii kuhusu suala hili.Mtoto akizaliwa na kupimwa HIV- kutoka kwa mama aliyepimwa HIV+ watu watasema mungu amefanya maajabu yake,watu wakisikia/kuona wanandoa wanaoishi wakati mmoja amepimwa HIV- na mwingine HIV+ bila kutimia 'kinga' kwa miaka mingi,watasema mungu ametenda maajabu,watu wakiona mtu aliyepimwa HIV+ na anaishi kwa miaka mingi bila kutumia ARVs napo watasema aidha ni carrier au mungu anamlinda au vipimo vilikosea.

Kuna mikanganyiko lukuki ipo kwenye jamii lakini watu wanajifanya hawaioni na hawataki kuhoji kabisa kutokana na mgando wa bongo zao.

Mwenye macho na aone.
 
Binafsi mkuu Deception nilipoona mada zako nikikuelewa, nilijituma na kusoma na kuangalia Documentaries usiku na mchana nilijaza laptop Yangu Documentary, sasa nami naamini HIV yupo ila ni retrovirus (harmless), UPUNGUFU WA KINGA hutokea yan UKIMWI ila hausababishwi na HIV au VIRUS na ninaamini ngono haiambukizi HIV ila najua UKIMWI upo kwasababu nyingine nyingi kulingana na Jeografia ya mahali, maisha na uchumi. MWISHO najua mtu anaweza kupona au kuondoa Tatizo la UKIMWI
 
Unajua mkuu,sio kila jambo linaweza kueleweka kwa kila mtu,lakini wakati najituma kuelezea suala hili nilijua wazi kwamba kuna watu 'potential' kama wewe ambao wangeweza kunielewa,ndio maana bado nilikuwa na nguvu ya kuendelea kutoa elimu hii pamoja na vikwazo vyote nilivyopata kutoka kwa wanajamiiforums wengine.

Ni jambo la kujipongeza kwa wewe kuwa hivyo kwa kuwa ni wachache sana wenye tabia kama yako ya udadisi.Wajanja wanasema,ukitaka kujifunza kitu lazima ukubali kusikiliza kwanza.

Ila nitarekebisha kidogo maneno yako hapo kwenye bold.Mimi huwa nasema kwamba hakuna kabisa HIV,kama ukimwi hausababishwi na kirusi hivyo basi,technically,hakuna kirusi kinachosababisha ukimwi,yaani hakuna HIV kwa maana ya kirefu cha jina lake.Hivyo ni sahihi pia kusema kwamba hakuna HIV.Najua utakuwa umenielewa vizuri sana.
 
Back
Top Bottom