Jamani neno "virusi" limeingia katika lugha.
Wengi huandika "Virusi vya UKIMWI", "virusi vya kompyuta".
Lakini hii ina matata. Nimeshaona watu wanaoandika "virusi vya kompyuta ni hatari; wiki iliyopita kirusi kipya..."
Hii naona haiwezekani kwa sababu "Kirusi" lamaanisha lugha pekee. Neno ambalo tumepokea kutoka Kiingereza katika Kiswahili ni "virus", si "kirus".
Hapa naona udhaifu wa kawaida hii;: namna gani kutofautisha kati ya virusi 1 (virusi kimoja? virusi vimoja ????) na virusi 100 (virusi vingi?).
Mnaonaje ? Tuseme virusi ya Ukimwi, virusi za hatari sawa na matumizi ya neno "video"?