Viongozi wetu mnatutia aibu kama Taifa

Blessed Jr

Senior Member
Nov 17, 2016
134
235
*VIONGOZI WETU, MNATUTIA AIBU*
Nioneshe masikitiko yangu sana kwa Viongozi wetu na Serikali kiujumla kwa jinsi mnavoshughulikia changamoto na kero za wananchi.

Serikali ipo kuwatumikia Wananchi, ibara ya 8.-(1)(a) inasema kuwa "Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii".

Na (b) inaseme, "Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi".

Na (c) nayo inasomeka kama ifuatavyo "Serikali itawajibika kwa wananchi".

Lakini Kipengere (d) nacho kinasomeka, "Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii".

Nimeweka vipengere hivi kisha nioanishe na jinsi Serikali yetu inavyojitajidi kupambana na changamoto za maisha ya Wananchi wake lakini kwa njia ambazo mara nyingine ni za *kilaana.*
Ni wazi kuwa wananchi wanawajibika kwa Serikali yao, kila mtu anawajibika kwa nafasi yake, Walimu wanawajibika, Madokta/Manesi, Wakulima, Wafanyabiashara n.k.

Kuwajibika kwa hawa watu kunaipa Serikali mapato ili kutengeneza mazingira rafiki ya kufanyia kazi na kuendesha Nchi. Japo viongozi wetu wamekuwa na dhana mfu kuhusu kodi, wamewarundikia wananchi utitiri wa kodi wakidhani ndiyo njia sahihi ya kupata mapato, badala yake imekuwa ni mzigo kiasi kwamba badala ya kumsaidia huyu mwananchi kuondokana na ugumu wa maisha mzigo umekuwa mara mbili zaidi na kushindwa kuchangia pato kwa nchi na nchi kubaki omba omba na *kutumia Rambi rambi* kama njia ya mapato.

Lundo la kodi kwa mwananchi ni mapato madogo kwa serikali, si mfanyabiashara wala mfanyakazi atakayemudu kuendesha maisha kwa kuwa anachobaki nacho baada ya kodi ni kidogo. Uzalishaji utakuwa mdogo, wafanyabiashara watafunga biashara, wafanyakazi watapata ujira lakini mtaani watakumbana na bidhaa kuwa ghali kwa kuwa wafanyabiashara aidha kama si kuongeza bei katika bidhaa kufidia kodi basi kwa uchache wa bidhaa sokoni italazimu bei kuwa juu.

Na hili la kodi ndilo linaloikumba nchi yetu, utitiri wa kodi kiasi kwamba kwa wafanyabiashara imekuwa changamoto, na kwa wafanyakazi hali kadhalika.

Matokeo ya utitiri wa kodi umezaa JANGA kubwa sana katika Taifa letu, *Rambirambi kutumika katika shughuli za maendeleo*, Serikali imeshindwa kukusanya kodi kutoka katika Migodi kwa mfano ili kuitumia kama chanzo cha maendeleo, leo hii wanatumia michango ya Rambi rambi katika shughuli za maendeleo. Ni aibu kama taifa, kwamba Viongozi wameshindwa kutafuta njia mbadala ya kukusanya kodi isipokuwa Rambi rambi au pesa za maafa.

Tulishuhudia Maafa ya Tetemeko la Ardhi Bukoba, waathirika wakiwa na imani ya angalau kurudisha makazi yao yaliyoharibiwa vibaya na tukio lile, matokeo yake Serikali ikaelekeza pesa zile kwenye shuhuli za maendeleo. Hatupingi maendeleo, tunapinga pesa zinazotolewa na watu tena kwa kujinyima kusaidia wenzao walio katika wakati mgumu kutumika sivyo. Hivi kweli Serikali inategemea maafa kuwahudumia Wananchi, kweli???? Taarifa ya *The Guardian* inaonesha migodi miwili tu Nchini ndiyo inayolipa kodi, kwa nini tusikusanye kodi huko tukafanya maendeleo? Hapa kuna tatizo la maono, Serikali yenye maono hafifu, Serikali ya kutumia Rambi rambi ni Serikali ya laana.

RC ananukuliwa akisema eti awaite wafiwa awaambie kuwa Milioni 59+ wakubali zielekezwe kuboresha Hospitali, haya ni maono hafifu, hii pesa ilitolewa na wanachi kwa ajili ya kuwafariji wafiwa na si kwa ajili ya kukarabati hispitali. Hii ni aibu kubwa sana, kwamba Serikali haina pesa za maendeleo mpaka wasubiri majanga yatokee ndo pesa iende huko. Hawa ndiyo viongozi wanaokaa mbele ya kamera na kusema eti, ningekuwa mimi ndiyo Rais ningewachapa, kwa kuwa tu wafanyakazi walibeba mabango ya kuonesha hitaji la kuongezewa stahiki zao. Viongozi ambao elimu zao zimetiliwa shaka nakushindwa kujitokeza na kulisemea. Tukiwa na aina hii ya viongozi tusitegemee miujiza, wamefeli, wakae pembeni, sifa ya uongozi hawana.
Serikali itafakari juu ya mambo haya ya kuombea maafa yatokee ndiyo pesa ipatikane ili waelekeze pesa hiyo kwenye maendeleo. Mwisho wa siku wananchi wataogopa kuwafariji wenzao kwa hofu ya serikali kujimilikisha pesa hizo. Ni aibu.
Viongozi mmetukosea na kututia aibu, mtuombe radhi na mbuni vyanzo vya mapato na si tutegemea pesa ya maafa, ni laanana, na hii laana haitatuacha salama kama taifa.
*PG*
 
Wana nyoosha kwanza ngoja tuendelee kuwasubiri wamalize kunyosha.
 
Hii ni laana kula pesa ya wafiwa, mwanadamu ukifikia sehemu ya kukosa soni, kukosa aibu wewe u sawa na hayawani.

Meseji senti!
 
Huyu alieshika usukani ndio chanzo wa haya yote yanayotokea.
Kama anadiriki kumkingia mtu kifua asiguswe, unategemea nini.
JP anavuta bangi sijui ?mbona haoni aibu anamlinda Bashite?na leo Daudi amemkana baba yake laana juu ya laana
 
Kama nchi inakuwa na mkuu wa mkoa kama Bashite, then tunakaa tunasubiria maendeleo basi hakyanani we are going backwards
 
Back
Top Bottom