Viongozi wengi hawaendi na kasi ya Dr Magufuli.

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Amini usiamini ndivyo ilivyo! viongozi wengi hawaendi na kasi ya Rais Magufuli na wengine hawajui wafanye nini.Angalia kwa mfano, Miji mingi imerudi kwenye hali ya uchafu, maeneo mengi hayafyekwi, takataka zimezagaa kila kona.Mimi nilitegemea wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wa maeneo ya kata na mitaa wangetengeneza utaratibu wa kudumu wa jinsi ya kusaidia manispaa na Halmashauri zao kudumisha usafi.lakini wapi wanategemea Rais awakumbshe tena.

Jambo jingine kwa mfano wanafunzi wa shule za msingi wanarudi nyumbani saa 8, hakuna masomo ya ziada baada ya hapo kwa kisingizio cha elimu bure hivyo viongozi wanaogopa hata kukaa na wazazi ili waangalie namna ya kuwasaidia wanafunzi hawa wasikae bila kazi muda mrefu kwan vinginevyo watafeli vibaya sana kwenye mtihani wao wa mwisho.najiuliza hivi Rais amewazuia kabisa kufikiri? amkeni viongozi, shirikisheni umma katika maeneo yenu ya kiutawala ili Nchi ipate maendeleo.
 
Nakuunga mkono, mkuu hata mimi huwanajiuliza maswali mengi kwa jamii yetu ila sipati Hivi.
 
Back
Top Bottom