Viongozi wakubwa wameamua kuharibu nchi yetu

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
222
529
Kuna mambo yanaongelewa "mtaani" (majukwaa yasiyo rasmi) ukiyasikia unaweza kudhani unaota au hayapo kumbe ndio uhalisia

Ukiona na kusikia wasanii wanaotunga tungo za kuikosoa serikali wanawindwa na vyombo vya usalama huku wanaotunga tungo za kuharibu kizazi kwa kusifia ngono na kuifundisha hadharani kwa vijana na watoto wanapongezwa na kupewa majukwaa makubwa unaweza usielewe kwa haraka haraka kwamba viongozi wanaandaa kizazi cha hovyo lakini huo ndo uhalisia

Ukiona vijana wa chuo kikuu wanakimbizana na kadi za CCM na kutwa kuchwa wanashinda na uniform na kofia za kijani, unaweza usielewa kwa haraka haraka kuwa nchi inaandaa vijana wa hovyo wa "kuabudu" binadamu wenzao wenye vyeo lakini huo ndio uhalisia

Fanya zoezi dogo tu, tafuta vijana kumi wanaosoma chuo kikuu chochote nchini kisha save namba zao za simu upate wasaa wa kuangalia status zao za watsap na profile picture zao utajua nachokisema

Vijana walioko masomoni wamelishwa sumu kwamba kama hauna kadi ya CCM haupati ajira serikalini hata kama una sifa za ziada

Vijana wametengenezewa mazingira ya kuamini kwamba "uchawa" na kujipendekeza kwa viongozi ndio njia rahisi ya kuyafikia mafanikio

Vijana wasomi wamegeuka kuwa "mazwazwa" kwa viongozi wao wa chama na kudidimiza uwezo wao wa kufikiri na kuchambua mambo

Siku hizi imekuwa vigumu kuwapata vijana wenye uthubutu wa kuhoji mambo mbalimbali ya hovyo yanayofanywa na serikali kwa kuhofia kesho yao

Walioko madarakani nao hawataki kuwajibika kwasababu hakuna watu wa kuwawajibisha

Wanasiasa wametengeneza machawa wengi ili kuepuka usumbufu wa kuhojiwa. Wanataka wafanye wanavyotaka wao

"Inasemekana" kumbe hata ajira za siku hizi zinazotangazwa watu wa selection wanapewa maelekezo ya kutembelea data base ya CCM kukagua wanachama wao walioomba wapewe kipaumbele

"Inasemekana" viongozi wa juu wa UVCCM hupita vyuoni mara kwa mara kuhimiza vijana wachukue kadi za chama ili wasijepata shida kupata ajira kwasababu siku hizi kadi zipo ki electronic! Hii ni ajabu na kweli lakini ndio uhalisia wenyewe

Msione siku hizi vionozi wa vyuo vikuu hawana makali katika kutetea haki za wanavyuo mkadhani hakuna wanachuo wanaopata shida, la hasha! Ni kwasababu wengi kama sio wote ni UVCC na wamepewa maelekezo ya kutoichafua serikali kwa kuanika shida za wanavyuo

Siku hizi warembo wa vyuoni wamekuwa rahisi sana kuangukia kwenye dimbwi la kuendekeza ngono si kwamba ni wahuni na wanapenda au wanamihemuko! Ni magumu wanayopitia hasa ukizingatia wanajua kabisa uhalisia wa familia walizotoka na jamii imeshaaminishwa mikopo ni asilimia mia kwa mia

Vyuo vikuu siku hizi vinaendeshwa na makada wa ccm ambao nao hawako tayari kuona serikali za wanafunzi zinaongozwa na watu wasio makada. Sifa mojawapo ya kuupata uongozi wa juu ni kuwa active member wa ccm

Si kwa ubaya, lakini aina hii ya uongozi ni kuharibu Taifa. Ni kuandaa vijana wasio wajibika. Tuwaandae vijana walioko tayari kuwajibika na kuwajibisha wasio wajibika

Kama CCM wanaharibu nchi, Wasomi wako kimya, wapinzani wamelala dolo, nani wa kulikomboa Taifa hili??
 
Haya yana mwisho ndg yangu japo inaweza kuchukua muda mrefu.

Tunahitaji wapinzani watano 5 tu wenye ushawishi usiokkuwa wa kawaida.

Kazi yao itakuwa ndogo sana.
Kazi kubwa ni kuigeuza nioyo iliyokata tamaa na kuijaza matumaini maoya, kuinua macho na kuiona Tanzania iliyibora bila ccm.

Kuitazamisha jamii jinsi ccm imedumaza akili na maendeleo.

Kuitazamisha jamii jinsi ccm inafaidi keki ya taifa kwa mtandao mzito.

Jamii ikishajazwa sumu ya mabadiliko zaidi ya ilivyokuwa 2015 hakika ccm imekwenda na maji.

SIKU YA MABADILIKO ITAKUJA KAMA UPEPO, TUOMBE UZIMA
 
Back
Top Bottom