Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,743
- 22,452
Viongozi na watendaji wa vyama vya msingi 49 wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, wamewekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanue Luhahula, kutokana na kushindwa kuwalipa wakulima.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na viongozi na watendaji hao, mkuu wa Wilaya amesema kitendo cha wao kushindwa kuwalipa wakulima fedha hizo inaonesha kuwa wamekula kwa sababu wanazozijua wenyewe, jambo ambalo linapelekea kuwagombanisha wakulima na serikali yao.
Amewataka viongozi hao kuhakikisha wanalipa fedha za malipo ya tatu kiasi cha sh. Bilioni 1.4. ndani ya wiki moja huku akimwagiza kaimu Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo ASP Faki Saidi,kutowaachia watuhumiwa hao mpaka walipe fedha hizo na atakae shindwa apelekwe gerezani wilayani Newala.
Akitoa ufafanuzi juu ya fedha anazodaiwa kiasi cha sh. Milioni 88, kiongozi wa chama cha msingi cha Mtoi AMCOS, Abdallah Mtoi, amesema fedha hizo ziliingizwa katika mikopo wakati wa uongozi uliopita kabla yake.