Mkutano wa 9 wa UVCCM, Dodoma: Rais Magufuli afuta bodi ya umoja wa Vijana! Awataka kutoogopa kujibu hoja za upinzani

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929




LIVE TEXT:

Mkutano Mkuu Maalum wa 9 wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) ukiendelea katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

====================================
Shaka: UVCCM imeendelea kuimarika zaidi, wanachama wamezidi kuongezeka kutoka zaidi ya Wananchama 800,000 hadi kufikia zaidi ya Wanachama 1,000,000"

Shaka: UVCCM imetoa takribani asilimia 75 ya Watu kwenda kufanya kazi kwenye jumuiya nyingine.

Shaka: Katika kipindi cha miaka 5 kuanzia 2012 hadi sasa UVCCM ngazi ya Taifa imefanya ziara kwenye mikoa yote nchini.

Shaka: UVCCM imeendelea kushiriki na kuwa chachu ya ushindi kwenye chaguzi mbalimbali za Serikali za mitaa 2019 na ule uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo CCM iliendelea kushika dola.

Shaka: Hata kwenye chaguzi ndogo UVCCM imeshiriki vilivyo na kuhakikisha CCM kinashinda kwa kishindo

Shaka: UVCCM ilianzisha Magufuli Club ambayo ilileta mafanikio makubwa kwenye uchaguzi Mkuu.

Shaka: UVCCM ina hakikisha ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 inafanikiwa.

Shaka: Jumuiya imeendelea kufanya uhakiki wa mali zake, kununua magari mawili mapya, kuruhusu jumuiya ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu

Shaka: Mheshimiwa Mwenyekiti CCM Dk. Magufuli tunaomba utupatie eneo katika mkoa wa Dodoma ili Jumuiya ya Vijana tufanye uwekezaji wa Kisasa

Mboni ; Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Dk. Magufuli kwa kufanikisha vilivyo Mkutano huu Mkuu wa Tisa (9)

Mboni: Tunakushukuru Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi unaofanya haswa unapolinda rasilimali zetu. Hakika wewe ni Mzalendo"

Mboni: Sisi Vijana tunakuunga mkono sana Mheshimiwa Rais Dk. Magufuli kwa kila hatua unayopiga tupo pamoja nawe

Mboni: Ninawashukuru Watu wote waliofanikisha mafanikio ya uongozi wangu kwa kipindi cha miaka mitano

Mtulia: Nashukuru kwa kupata fursa hii ya kujiunga na CCM

Mtulia: Nimeacha kila kitu na kuamua kujiunga CCM kutokana na mapenzi yangu binafsi kwa CCM na kwa matendo mazuri ya utendaji unaofanywa na Dk, Magufuli
Mtulia: UVCCM iendelee kuwa mkombozi na mlezi wa vijana na makundi yoyte ya vijana nchini

Moses Machali: Nimeamua mimi na wenzangu kujiunga CCM ilipo timu ya ushindi

Moses Machali: Siasa zimehamia mitandaoni. CCM tulikuwa tumelala, nashauri tuamke! Vyombo vya Habari vinaweza kufanya mazuri kuonekana mabaya na mabaya kuonekana mazuri. Twende mitandaoni tukapambane na wapinzani wetu!

Machali; Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli usikatishwe moyo na wala wanachama msikatishwe tamaa mnaposikia tumenunulia, wanaosema hivyo ni wadhaifu sana.

David Kafulila: Nimeamua kuhamia CCM kwa sababu Ajenda ya Ufisadi imehama. Sasa kuna utu na usawa nchini.

David Kafulila: Tanzania ya sasa imebadilika. Tunashuhudia matajiri wakiwa lazwa mahabusu. Hii imepelekea kiwango cha ufisadi kupungua nchini.

David Kafulila: Dhamira ya Dk. Magufuli haina mashaka, Uzalendo wake ni wa kuigwa mfano.

Albert Msando: Ni wajibu wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM kuchagua viongozi walio wasafi na wachukia ufisadi na rushwa. Msichague mtu sababu mnatoka ukanda mmoja!

Albert Msando: Vijana ni wajibu wenu kujiandaa kujibu hoja za wapinzani. Na ili muweze kujibu hoja ni lazima muwe na maarifa ya kutosha kuhusu anachokifanya Rais wetu na Serikali kwa ujumla

Albert Msando: Tujenge UVCCM inayoweza kujibu hoja kwa hoja. Nimeona mmeandika kuwa kuna wanachama wa UVCCM milioni 6; lakini idadi iliyoandikwa kwenye kitabu kingine mnaonyesha ni wanachama 1,547,000! Tusimdanganye Rais..

Albert Msando:Wapinzani siyo tu wanapotezana, bali hadi sasa wameshapotezana, tumeshawapiga 4-0 ugenini na tukirudi nyumbani nako ni 4-0, tunamaliza kazi -

Patrobas Katambi: Tusiruhusu watu wengine kutumia nafasi nyingine za kidemokrasia kuvuruga amani ya nchi yetu. Nilipokuwa CHADEMA, niligundua yaliyokuwa CCM ya zamani yamehamia CHADEMA!

Patrobas Katambi: Hivi, viongozi wa upinzani wakipewa nchi nani wanaweza kuunda serikali? Kama wanashindwa kusimamia bajeti ya msiba, wataweza kusimamia bajeti ya Taifa?

Patrobas Katambi: Hivi, viongozi wa upinzani wakipewa nchi nani wanaweza kuunda serikali? Kama wanashindwa kusimamia bajeti ya msiba, wataweza kusimamia bajeti ya Taifa?

Patrobas Katambi: Nikitazama Katiba ya CCM na CHADEMA nimeona kuna tofauti chama nilichokipigania kinageuka misingi yake na kuanza kupokea wala Rushwa, Mafisadi pamoja na matumizi Mabaya ya Ruzuku.

Patrobas Katambi: Wale walioongoza mapambano dhidi ya Ufisadi (Zitto, Dkt. Slaa, Kafulila etc) hawapo tena CHADEMA. Wale waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ndo wamehamia CHADEMA!


Rais Magufuli

Rais Magufuli: Mimi ninaamini sana vijana, mkiamua jambo mnaweza. Bahati mbaya sana kuna wachache mlipotezwa na watu flani flani hapa kati.

Rais Magufuli: Ningependa ieleweke, ujana pekee haukufanyi uwe hazina kwa chama au taifa. Ni lazima uwe mzalendo, mchapakazi, muadilifu na kadhalika > Hizo ndizo baadhi ya sifa za kijana

Rais Magufuli: Kijana ambaye ni fisadi, mvivu, mla rushwa, tapeli, mtumia dawa za kulevya na kadhalika, ana mchango mdogo kwa taifa - Nimeanza kueleza kwa kutaja sifa hizo za kijana kwa makusudi kabisa

Rais Magufuli: UVCCM ya zamani sio sawa na hii ya sasa. Vijana wa sasa wanaenda kwenye mikutano wanapigana, wengine wanatoa rushwa. Ninapozungumza hapa tu Mwenyekiti wenu yupo Lock-up kwa kushikwa na Rushwa > Huo ndio umoja wa vijana tuliokuwa tunaenda nao

Rais Magufuli: Niwaeleze ukweli, vijana walinisaidia sana wakati wa kampeni lakini nashangaa nimekuwa nikiletewa majina ya wanaopendekezwa kwa nafasi mbalimbali, ila sikuletewa hata jina moja toka UVCCM!

Rais Magufuli: Mimi nasema ukweli hata Mungu ananisikia, sikutoa hata senti moja ili nichaguliwe > Nitashangaa sana kama mtamchagua Mwenyekiti aliyewahonga.

Rais Magufuli: Kila mwenye uwezo kwenye umoja wa vijana, amewekewa vigingi vya kila aina, nawaomba wajumbe tuanzishe ukurasa mpya wa Umoja wa Vijana

Rais Magufuli: Kuonesha ni kiasi gani ninavyowaamini vijana, kwenye serikali yangu nimeteua vijana wengi na hawajaniangusha

Rais Magufuli: Usichague mtu kwa sababu ya dini yake, kabila lake, mnatoka ukanda mmoja au pesa zake > Chagua mtu ambaye ni sahihi na ana sifa za kuwa kiongozi

Rais Magufuli: Ninawaomba vijana wa UVCCM mjitambue. Huu ni wakati wenu wa kushika dola. Nisingependa kuona sisi tunaondoka halafu anachukua kijana anayechukua rushwa...tutakuwa tumeliuza taifa hili na kukiuka misingi tuliyoachiwa na waasisi wetu

Rais Magufuli: Mimi sio Rais wa maisha, muda wangu utaisha. Dkt. Shein naye muda wake utaisha na hiki ni kipindi chake cha mwisho - Nataka vijana mtambue hili taifa ni lenu

Rais Magufuli: Vijana wa CCM naomba mjiamini. Muwe mnajibu hoja, msisubiri kuambiwa > Bahati nzuri mimi huwa nasoma, nimemuona Msando akitumia taaluma yake ya sheria kujibu hoja kuhusu Ibara ya 45 jana na sikumtuma
 
Wakuu
Mkutano Mkuu wa tisa wa UVCCM tayari umeanza katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.Mh Rais Dk John Magufuli muda wowote ule atatoa hotuba ya ufunguzi.
1. Mh David Kafulila anaongea na WanaCCM baada ya kukaribishwa rasmi. Anataja sababu za kuhamia CCM
Agenda ya ufisadi imehama kutoka kwa wapinzani.
JPM ndio Rais wa mfano kwenye kupambana na ufisadi barani Afrika.
Misingi ya TANU ya Utu na Usawa imerudi.
2. Albert Msando anaongea baada ya kukaribishwa rasmi.
UVVCCM waache kuendekeza rushwa.Kuna wajumbe wamepokea rushwa.
Wajumbe wasichague wala rushwa bali wachague viongozi wenye uwezo.
UVCCM waache kumdanganya Rais kwa kupika takwimu za idadi ya Wanachama
Makundi yote yavunjwe mara tu baada ya uchaguzi.
3. Patrobas Katambi anazungumza
Tusiruhusu watu waharibu amani ya nchi kwa kutumia fursa ya demokrasia iliyopo.
Vijana wawe nyuki na wasiwe nzi.
Ametoka kuwa mgambo amejiunga na JWTZ
Upinzani ukipewa serikali nani atakuwa Waziri?!
Hati yenye mashaka kila mwaka
Watoe ushahidi wa CCM kununua wanachama.
Tuungane kwa pamoja
Utambulisho wa vyama vya siasa vilivyoleta wawakilishi
NRA
TLP
CCM
ADC
UDP
Chauma
UMD
Vyama rafiki
Frelimo
ZANU PF
Sasa Mh Rais John Pombe Magufuli anazungumza
 
Nonsense...
c18c0afdacd1c794ade40610e70a96fc.jpg
 
Naona mnahimizana kumezesha wananchi propaganda kwenye mitandao ya kijamii....you guys are tired physically and mentally
Na hiki ndicho kinachowapa kichwa upinzani ya kuwa wanakubalika.

Wanajisahau kuwa vijijini hawajawekeza chochote zaidi ya kauli ya itamwagika damu.

Ukimtaka MTU aokoke huku unamwambia hajielewi kiakili huko aliko.

Huchukua hatua fupi kujitofautisha yeye na wewe nani hana akili.
 
Back
Top Bottom