Viongozi wa UKAWA, na msiende peke yenu.

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Amani kwenu wanaUKAWA.
kwanza nawapongeza sana kwa kutoa changamoto stahiki kwa chama tawala. Hata hivyo nina machache ya kushauri.

Kwanza naomba mfahamu ya kwamba kila zama na kitabu chake. Katika awamu hii ya tano inayoongozwa na JPM naomba muwe wabunifu sana kuendesha harakati za kisiasa. Kwanini?

1. Mengi ya mambo anayo yafanyia kazi JPM yametokana na kelele za upinzani -ukawa ninyi wenyewe.
2. Magufuli ana msimamo ni mtu asiyeyumbishwa.

Hivyo niwaombe muandaye sera mbadala mtakazo zisimamia na kuonyeaha utofauti dhidi ya ccm. Msikimbizane na matukio ya serikali ya jpm. Matukio yq jpm yana malengo ya kujenga taifa lililo bora ambayo ninyi ndiyo mmekuwa mkipigia kelele.

Punguzeni kutoa ahadi za kuzunguka nchi nzima kuisemea serikali kwa wananchi halafu mnaishia kufanya mkutano mmoja tu na kupotezea. Kwa kufanya hivyo mnapoteza uaminifu.

Jambo la mwisho lkn si kwa umuhimu ni kwamba siku zote kama kuna jqmbo/tukio mnataka kushughulika nalo basi hakikisheni hamlibebi wenyewe. Pandikizeni kwa wananchi, wajawe na hasira halafu wao ndiyo waishinikize serikali. Mkilibeba wenyewe mnaonekaba mnatafuta umaarufu ama huruma ya kisiasa.

Kuwe na ajenda ama sera mbadala ambazo mkiziweka masikioni mwa wananchi ziwapeleke mbio na kuwafuata. Mkifanya hivyo hata serikali itawaogopa maana itajua nyuma yenu kuna nguvu ya umma.

Kususa hakusaidii chochote. Mmeona ktk bunge maalumu la katiba kususa hakukusaidia. Pia mmeona ktk uchaguzi wa marudio Zanzibar kususa hakukuwasaidia CUF.

Ni hayo tu.

Wenu KIGODORO.
 
Back
Top Bottom