Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Jeshi la Polisi mkoani Songwe linawashikilia viongozi watatu akiwemo mwenyekiti, balozi na Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Maninga wilayani Mbozi kwa kushindwa kutunza hifadhi ya msitu wa asili katika pori la Maninga lililiovamiwa na watu wasiojulikana ambao wamesababisha uharibifu mkubwa kwa kukata miti ya asili na kinyume cha sheria.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Songwe Mathius Nyange amesema msitu huo uko kwenye hifadhi ya kijiji na kwamba wenye dhamana ya kuulinda ni viongozi wa kijiji ambao mpaka hivi sasa wanashikiliwa na jeshi hilo wakidaiwa kufanya uzembe kwa kushindwa kuutunza msitu huo hivyo watatakiwa kutaja ni nani waliwapatia vibali vya ukataji miti katika hifadhi hiyo.
Aidha Kamanda Nyange amesema jeshi lake kwa kushirikiana na idara ya maliasili limefanya operesheni katika hifadhi ya msitu huo na kubaini uharibifu mkubwa kutokana na ukataji miti ya asili jambo alilosema linatishia uhai wa msitu huo wa asili, huku afisa misitu wilaya ya Mbozi Zakayo Mwamahonje akitaja kuwa jamii ya miti inayokatwa ni adimu na kwamba bado ipo katika hatari ya kupotea, hivyo idara yake itahakikisha inawakamata wahusika wa biashara ya miti hiyo na kuwafikisha kwenye vyombo husika.
Operesheni hiyo imeibua taharuki baada ya jeshi la polisi kunasa shehena ya magogo 215 yaliyovunwa kinyume cha sheria na kufichwa kwenye kaya ya mfanya biashara mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi. Ambapo wakazi wa kata ya Bara wanadai hawajawahi ona biashara kama hiyo katika maeneo yao.
Chanzo: ITV