Viongozi wa kambi ya upinzani ni wachovu wa fikira. Wanahitaji mabadiliko!

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
SIASA.

( Dr. Muhammed Seif Khatib)

Kila mtu anaipenda siasa na kuitamani. Ila malengo ya kila mtu ya namna ya kuitekeleza huwa tofauti. Kila mwanasiasa atajigamba kuwa anaingia katika siasa ili kuwatumikia wale waliomchagua au watakaomchagua. Mtu wa aina hii ukimtazama usoni, nafasi yake inamsuta. Kwani kuwatumikia watu lazima uwe katika siasa? Mtu huingia katika siasa kwa kuamini huko ndiko kwenye neema. Vipo viriba vya maziwa na vibuyu vya asali.

Mishahara minono, marupurupu pomoni na viinua mgongo Chekwa. Kama hilo ndoa la kweli la masilahi kwa nini Waheshimiwa wawe walafi? Huomba rushua. Fedha wapewazo hazitoshi? Wakiwa Mawaziri Wakuu wanachota! Wakiwa Marais wanasomba! Wakiwa Mawaziri wanakomba! Au mishahara ni miduchu! Kama ni hivyo ngapi zawatosha? Tukiacha hawa, vipi matajiri na wafanyabiashra wakubwa nao huingia siasa.

Nao wanafatia mishahara na posho za kukaa vikaoni? Unaweza kulinganisha mitaji yao, mali zao na mapato yao na walipwacho katika siasa? Muda wanawatumia katika siasa na wangeutumia katika biashara zao, upi wenye tija kimasilahi.

Wote hawa wanaoingia siasa wale wanaomaliza huko maisha yao huwa bora kuliko walivyoingia? Huwa na mali zaidi? Huishi kwa kula na kunywa tu bila kufanya kazi? Nini hatima ya wale wanaopata ajali za kisiasa? Haiba yao, heshima na utu wao huwaje? Utumishi ulotukuka kwa waloowachagua huwaje? Lipo kundi la wastaafu kutoka amali mbalimbali. Majanarali na mabregadia kutoka jeshi.

Makamanda na maenspekta kutoka polisi. Wakurugenzi na mameneja wa makampuni. Wote hawa huivamia siasa. Wanafata nini? Kuwatumikia wananchi katika uchovu na kukongoroka? Bila ya shaka nao wanafatia pesa. Huko zivururu? Walikotoka hazikuwepo za kutosha. Na viinua mgongo havitoshelezi. Wapo wataalamu, shababu na shakii.

Siyo wazee siyo wastaafu, ni wabichi wanatoka utomvu wa uzima. Madakitari wa binadamu wameziacha thieta na wagonjwa vitandani kuingia siasa. Maprofesa wameyakimbia madarasa vyuoni kutia vitabu kwapani kuhangaika na Siasa.

Watoa haki mahakamani na watetezi wa washitakiwa wamevua suti na tai zao, hawana mbwembwe na matao, sasa wanacheza siasa. Kundi la magabachori, wengine hata Kiswahili hawajui nao wamecharuka siasa kuivamia. Magolo polepole wanawaengua.

Majukwaa ya wasanii, safu inapungua, usanji unaelekezwa katika uwanja wa siasa. Kundi la wachungaji wameacha kueneza neno la Mungu na wameasi kumtumikia “Bwana”. Wameamua kuitumikia “shetani” - siasa. Waandisi wa umeme, ujenzi na maji wametelekeza taaluma zao. Wote wamejilundikiza siasani. Utaalamu unakosekana.

Maghorofa yanaporomoka kwa ukosefu wa utaalamu. Wacheza disko, wauza pombe na wamiliki wa vilabu vya usiku sasa ni viongozi wa vyama vya siasa. Hawa ni watoa sera, miongozo kwa wafuasi wao.

Mchanganyiko huu wa aina ya watu wanaoingia katika siasa kila mmoja na dirisha au mlango wake unatija? Vyama vya siasa vinakosa manahodha na marubani weledi. Nini tutarajiye katika saladi za wanasiasa wa aina hii na viongozi wao “wanaharakati”? Wataalamu wa tasnia ya siasa wanatwambia kuwa baada ya uchaguzi katika nchi ya kidemokrasia na Utawala wa sharia, siasa za vyama zinahamia bungeni.

Wawakilishi wa wananchi wakiwa bungeni ndipo kwenye hoja ipingwayo au kuungwa mkono kwa hoja. Wapiga kura sasa wanakuwa watazamaji huku wameshika kalamu zao na daftari wa kimtathmini kila mwanasisa asemacho na atendacho. Wanavitathmini vyama vya upinzani katika kukosa serekali. Wanakitazama Chama tawala katika kutekekeza ilani yake.

Katika mwaka wa kwanza wa siasa za vyama kuhamia bungeni imedhihirika kuwa ile saladi ya wanasiasa inayoongozwa na kundi la wanaharakati na wamiliki wa vilabu vya usiku haitekelezwi. Baada ya kushindwa kujipanga kwa hoja ndani ya bunge, genge la wanasiasa hawa kama kundi la mifugo lilokosa mchungaji limetoka bungeni kwenye malisho na kuzurura mitaani kuokoteza. Majukwaa ya siasa yanafungwa nje ya bunge.

Badala ya kuhutubia bungeni ili wasikike na kila mtu, sasa wanatakiwa kupiga kwata ya maandamano. Majukwaa ya siasa nje ya bunge yamegeuka membari za matusi.

Wafuasi wao hayo wanayoyataka kuwaambua mitaani wangeweza kuyatolea bungeni. Zipo njia kadha za kuyasemea kwa taratibu halali za kibunge. Viongozi wa kambi ya upinzani ni wachovu wa fikira. Wanahitaji mabadiliko!
 
Mleta mada ni janga,unasema badala ya kuhutubia bungeni wasikike na kila mtu wamekimbilia mitaani!. Bunge si mmefunga la ndani kwa ndani wanyonge hatuwaoni tena huku duniani. achaneni unafiki , kila lenye mwanzo lina mwisho. Nasema kila siku wenzetu wachache wanao pata nafasi ya kutunga taratibu na sheria wasijisahau kwa kuwa siku moja watatoka huko, wako wapi akina Sumaye, Lowassa,Mahanga, nk.sheria mbaya walizo zi shadidia wakiwa huko zinawakula na wao.
 
Back
Top Bottom