Viongozi wa dini kemeeni kauli hizi

Viongozi wa dini kemeeni kauli hizi

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,210
Reaction score
4,178
ndugu zangu watanzania, hakika ile nchi na chama ambacho Baba wa taifa ilikiacha kimeshatoweka na nchi inaelekea kusambaratika,

Baba wataifa aliijenga nchi ihi kwa misingi ya umoja na mshikamano, bila kujali dini au ukabila,

watanzania kwa miaka yote tuliishi kama ndugu, hakuna mtu aliye mwuliza mwenzake wewe kabila gani, au dini gani, tuliishi kama ndugu, kila mtu alioona fahari kumwita mwenzake ndugu,

wazee wetu waliijenga misingi ihi kwa gharama kubwa sana, wali liunganisha taifa katika misingi ya undugu na ujamaa:

sasa ni miaka 16 tangu baba wataifa alipoitwa mbele za haki,

sasa misingi ile ambayo baba wataifa aliipigania siku zote za uai wake, inabomolewa tena mbaya zaidi na chama alicho kiasisi mwenyewe,

leo viongozi wa chama cha mapinduzi, bila woga wanaivunja misingi iliyo lisimamisha taifa hili kwa miaka 50 na kuwafanya watanzania tuishi kwa amani,

chama kimepoteza mwelekeo, hakina sera tena za kuwaletea watanzania maendeleo,

kinatafuta madaraka kwa garama yeyote, iwe kwa kutugawa na kulivunja taifa bila kujua athari ya matokeo ya siasa hizo,

hai ingii akilini viongozi wakubwa tena walio heshimika sana na wananchi kusimama majukwaani na kulipasua taifa kwa kutamka maneno ya uchochezi na uvunjifu wa amani umoja na mshikamano wa taifa?

Mwaka 2010 walikuja na propaganda za udini, na hili limesha sambaza sumu kubwa sana kwa udini unaolitafuna taifa kwa sasa kuliko letwa na siasa uchwara za ccm,

sasa mwaka uhu wamekeja na propaganda za ukanda na ukabila, na sote jana tumeshuhudia viongozi wakubwa wakisimama majukwaani na kumwaga sumu hiyo na matusi,

ccm isifikirie kwa mchezo uhu italiacha taifa salama, na wala isijidanganye, yenyewe itabaki salama,

nawala wanaccm wanaoshabikia ujinga uhu wasijidhanie nawao watabaki salama, kwa uroho wa madaraka wa viongizi wao wanao tumia kila mbinu chafu za kubaki madarakani kwa kulipasua taifa,

hakika siyo upinzani utakao lisambaratisha taifa hili bali taifa hili litapasuliwa na chama cha mapinduzi chenyewe,

wito wangu kwa watanzania na viongozi wa dini:

siyo vyema kufumbia macho mambo haya yanayofanywa na chama cha mapinduzi,

tukemee kwa nguvu zote kauli hizi na kuwakataa watu hawa kwa kuwaondoa madarakani kwani tukiendelea kuwa acha taifa ili lita angamia kabisa,

naomba kuwasilisha, tuchangie kwa kina jambo hili bila ushabiki,
 
unawaomba viongozi wa dini wakati wenyewe ndo wapo nyuma ya kila mpango ovu......umeambiwa sumaye ameombwa na maaskofu wa KKKT sabab raisi wanataka atoke KKKT? ts Roma against KKKT. Wapumbavu na malofa pekee ndo hawajui chochote
 
kaka tusiongelee mambo ambayo hatuna ushaidi nayo, ihi ni michezo ya ccm kuwagawa wakatoliki na walutherani,

ili iwapate wakatoliki kama ilivyofanya 2010 kwa kuwachonganisha wa islam na wakaroliki, kwa kumwita dr slaa ni padri na ametumwa na wakatoliki,

tunapo ongea mabo haya nikwa afya ya taifa kaka kama wewe ni ccm jitafakari mara 2 je! Ihi ndiyo ile ccm ya nyerere?

Mimi naongea haya maana naifahamu sana ccm ile ya awamu ya kwanza maana nilibaatika kuwepo, na ndio maana nimeiongelea misingi iliyo jengwa kipindi kile,
 
Usijifanye kipofu usiyeona yanayofanywa na viongozi wa madhehebu ya kilutheri na Pentekoste. usojifanye Yale maandamano yao ya kwenda nyumbani kwa Lowassa Dodoma wakifanya na maombi hukuyaona. usijifanye hukusikia Pengo alivyojaribu kuonya Gwajima alivyomshughulikia. MAHABA YASIKUE
 
Wanayataka wenyewe afu wanaanza kulia leo hii na bado walitegemea nini kumtukana mzee Pengo au wanafikiri watz ni wajinga hawajui wanachokifanya hii sumu waliipandikiza wenyewe wacha mwaka huu iwatafune
 
ndugu zangu watanzania, hakika ile nchi na chama ambacho Baba wa taifa ilikiacha kimeshatoweka na nchi inaelekea kusambaratika,

Baba wataifa aliijenga nchi ihi kwa misingi ya umoja na mshikamano, bila kujali dini au ukabila,

watanzania kwa miaka yote tuliishi kama ndugu, hakuna mtu aliye mwuliza mwenzake wewe kabila gani, au dini gani, tuliishi kama ndugu, kila mtu alioona fahari kumwita mwenzake ndugu,

wazee wetu waliijenga misingi ihi kwa gharama kubwa sana, wali liunganisha taifa katika misingi ya undugu na ujamaa:

sasa ni miaka 16 tangu baba wataifa alipoitwa mbele za haki,

sasa misingi ile ambayo baba wataifa aliipigania siku zote za uai wake, inabomolewa tena mbaya zaidi na chama alicho kiasisi mwenyewe,

leo viongozi wa chama cha mapinduzi, bila woga wanaivunja misingi iliyo lisimamisha taifa hili kwa miaka 50 na kuwafanya watanzania tuishi kwa amani,

chama kimepoteza mwelekeo, hakina sera tena za kuwaletea watanzania maendeleo,

kinatafuta madaraka kwa garama yeyote, iwe kwa kutugawa na kulivunja taifa bila kujua athari ya matokeo ya siasa hizo,

hai ingii akilini viongozi wakubwa tena walio heshimika sana na wananchi kusimama majukwaani na kulipasua taifa kwa kutamka maneno ya uchochezi na uvunjifu wa amani umoja na mshikamano wa taifa?

Mwaka 2010 walikuja na propaganda za udini, na hili limesha sambaza sumu kubwa sana kwa udini unaolitafuna taifa kwa sasa kuliko letwa na siasa uchwara za ccm,

sasa mwaka uhu wamekeja na propaganda za ukanda na ukabila, na sote jana tumeshuhudia viongozi wakubwa wakisimama majukwaani na kumwaga sumu hiyo na matusi,

ccm isifikirie kwa mchezo uhu italiacha taifa salama, na wala isijidanganye, yenyewe itabaki salama,

nawala wanaccm wanaoshabikia ujinga uhu wasijidhanie nawao watabaki salama, kwa uroho wa madaraka wa viongizi wao wanao tumia kila mbinu chafu za kubaki madarakani kwa kulipasua taifa,

hakika siyo upinzani utakao lisambaratisha taifa hili bali taifa hili litapasuliwa na chama cha mapinduzi chenyewe,

wito wangu kwa watanzania na viongozi wa dini:

siyo vyema kufumbia macho mambo haya yanayofanywa na chama cha mapinduzi,

tukemee kwa nguvu zote kauli hizi na kuwakataa watu hawa kwa kuwaondoa madarakani kwani tukiendelea kuwa acha taifa ili lita angamia kabisa,

naomba kuwasilisha, tuchangie kwa kina jambo hili bila ushabiki,
Umesema tuweke ushabiki pembeni sawa, Walicho kifanya wana CCM kutoka kanda anayotoka ENL ni kipi? Kauli zao za jazba baada ya Mgombea wao kuto tosha zimedhihirisha wazi jambo hilo, uzuri walipokuwa wakiondoka hawakuondoka kimya kimya waliita vyombo vya habari na kuutangazia umma wa watanzania azma yao hiyo. Huku wakijua wazi watanzania wanasikia, wanaona na wanauwezo wa kufanya uamuzi sahihi. Watu walikuwa wakichekelea bila kukemea, walifurahi wakijua ni faida kwao, bila kujua upepo ukigeuka ni kilio.
Tunajua kwamba kila kundi, kabila dini na hata jinsia watataka Rais atoke kwao, lakini watanzania hawataki bora Rais, Tunataka Rais bora atakae kuwa muwajibikaji, atakae ondoa kero za watanzania kwa ujumla wake.
 
unawaomba viongozi wa dini wakati wenyewe ndo wapo nyuma ya kila mpango ovu......umeambiwa sumaye ameombwa na maaskofu wa KKKT sabab raisi wanataka atoke KKKT? ts Roma against KKKT. Wapumbavu na malofa pekee ndo hawajui chochote

acha kuzusha mambo kulichafua kanisa, na Mungu akufungue kwa jina la Yesu
 
11880374_738551432923428_3510802968194476253_n.jpg

Na bado, jana wanachama waliokuja ni milioni mbili tu wa DSM
 
Muammar gaddafi Aliwapa kila kitu wananchi wake,
Mwisho wa siku ukabila na Ukanda ukaiingiza Nchi ya libya katka Machafuko.
Libya ilikuwa na Amani ya kutosha,
Libya ilikuwa inakopesha nchi za Afrika,

Uchumi wa libya ulikuwa Mkubwa,
Watu wachache kwa manufaa yao wameivuruga ile nchi ili wateke Rasilimali zake,
Wakawadanganya wanaNchi kwa kuwatenganisha kwa Ukanda na ukabila,
Wananchi wakaamini,
Leo hii wanajuta
kweli kweli,
wale waliokuwa
wanapata kila kitu
Sasa hivi wanakimbilia
Ulaya kutafuta maisha
Bora ya Ukimbizi,
Rasilimali zao zimetekwa na wajanja waliopandikiza Chuki ya Ukanda na Ukabila,

Watanzania
hawadanganyiki kirahisi hivyo
Watachagua Ccm na magufuli,
Maendeleo yanaonekana,na ni Makubwa,
Na Magufuli atayaendeleza,
Mapungufu madogo madogo yapo maana tuko Duniani Mbinguni pekee ndo kuna wakamilifu,
lakini sio et Ccm
Haijafanya kitu ni mjinga tu ndiye atakayesema hivyo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

EPUKA MAFISADI
CHAGUA MAGUFULI.
 
nafikiri ushabiki mwingine sasa umepitiliza ugonvi wa madhehebu haya umeanza lini mwogopeni mungu
 
acha kuzusha mambo kulichafua kanisa, na Mungu akufungue kwa jina la Yesu

Mimi sikubaliani na swala la Udini.Ishu hapa ni ukanda na pioneers n wafanya biashara wa Kichaga.Hayo mambo yapo.Kinyume na hapo, Lowasa hana sifa hata moja ya kuwa Rais wa nchı.
 
Back
Top Bottom