Viongozi serikali za mitaa Tanzania ondoeni usingizi

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Wenyeviti wa mitaa/vitongoji na vijiji na watendaji wa kamati katika kata mnakuwa mizigo mno kwa wapiga kura wenu. Hivi ni kwanini nguvu mnayokuwa nayo wakati mnaomba kura inaisha kabisa mkisha chaguliwa? tuwaite wazenbe, wasaliti ama hamjitambui?.

Mfano, kuna maagizo mengi sana ya serikali toka huko juu lakini yakifika huku chini kwenu, kwa wananchi wa chini yanakosa usimamizi kana kwamba hamupo.

Juzi rais alionesha mfano akawaambia nini maana ya usafi kwa vitendo tukitarajia kuanzia hapo mitaa itachukua hatua hiyo kama sehemu ya wajibu wenu lakini hajabu leo ukipita kwenye mitaa ndo utashangaa ambavyo uchafu mpya umezagaa, unajiuliza wenyeviti tuliowachagua wanasubiri tena rais awakumbushe?.

Hiyo iache, juzi tu waziri wa afya kaagiza ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwakatwa kusaidia kupambana na kipindupindu lakini we pita barabarani uone, si ubungo, buguruni, makumbusho, kimara n.k.

Sehemu zote hizi yamejaa mananasi, machungwa n.k yaliyomenywa na yako wazi, unajiuliza watendaji wa chini kwanini mna usingizi wa kiasi hiki? Kwani nyie ni viongozi wa nini hasa? ama mnasubiri waziri aje mwenyewe kukamata? hebu timizeni wajibu wenu, madaraka matamu lakini mnatakiwa kuwajibika kwa jamii zenu pia.
 
Juzi nilienda kumtembelea dada yangu mitaa ya mbezi beach, nssf road nokasikia vijana wanavyomlalamikia mtendaji na m/kiti wa huo maa jinsi walivyofisidi hela za barabara, mtrndaji wanasema alivyokuja alikuwa na miguu sasa hivi ana vigari vyake viwili, nasikia Mbunge wa hapo ni halima mdee, sijui kwa nini halioni hili jambo
 
Inakuwaje raisi na mawaziri watoke ofisini ila hawa wakae tu maofisini wiki nzima, kwanini wasiingie mitaani kwao wakaratibu shughuri zao? hivi tuliwachagua wakakae tu maofisini hawa wiki hadi wiki, mwezi hadi mwezi? Huu ni ubwanyenye aisee, ni lazima tuwadhibiti kwasababu walitaka wenyewe hizo nafasi zao, ni lazima tuwabane sasa. Unayajuaje matatizo ya watu wako kama hutoki kuzunguka eneo lako la kazi? Hawa ndo wanatuletea kipindupindu na mambo mengine ya hovyo
 
Kwa kweli huku chini watendaji wamelala kabisaa utafikiri hawapo. Wanasubiri buku mbili mbili za kuandikia wananchi barua za dhamana, benki, kitambulisho etc
 
Back
Top Bottom