Viongozi CHADEMA wazuiwa kuingia ofisini Shinyanga

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Viongozi na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini Mwanza leo wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.

Waliokumbwa na adha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji na wabunge Godbless Lema, Ester Bulaya, John Heche, Halima Mdee na viongozi kadhaa wa kitaifa wa Chadema.

Magari manne ya polisi yaliyosheheni askari waliobeba silaha na mabomu ya kutoa machozi yaliupokea msafara wa Chadema uliokuwa ukielekea Mwanza, mara tu ulipoingia mjini Shinyanga na kuusindikiza hadi nje ya mji kuhakikisha hausimami ndani ya mji huo.

My take
Tunapoelekea sio kuzuri. Inatumika nguvu kubwa badala ya busara.
 
Nyerere alisema atakayeiangusha CCM atatoka humohumo. Naona unbii umekamilik.
"Maguful with the fall of CCM"
Amekuwa Magufuli tena, badala ya hawa jamaa tulioaminishwa mnamo September/October 2015 - kuwa hio quotation ya Nyerere iliwahusu hawa:-
1. Lowasa
2. Sumaye
3. Kingunge
4. Mwapachu, ila yeye akiri zimemrudi
5. Msidai
6. Mgenja.
 
Amekuwa Magufuli tena, badala ya hawa jamaa tulioaminishwa mnamo September/October 2015 - kuwa hio quotation ya Nyerere iliwahusu hawa:-
1. Lowasa
2. Sumaye
3. Kingunge
4. Mwapachu, ila yeye akiri zimemrudi
5. Msidai
6. Mgenja.

Tuvute subira...huko mbeleni naamini historia itakuja kuthibitisha kwamba hao uliwaorodhesha walitoa mchango kwenye anguko la ccm.
 
Hizi nchi za Kiafrika hizi,kwa kudhibiti wapinzani zina rekodi zilizotukuka.Lakini majizi yanayofilisi nchi kwa kutumia peni yanapulizwa na viyoyozi.Sikwambii majambazi yanayotumia silaha wanavyotamba.Intelijensia ya kung'amua wapinzani kuhatarisha amani ni kali sana lakini kuwagundua wanaohatarisha usalama wa taifa ni mpaka ipigwe ramli.Hiyo ndio Afrika ya wateule.
 
Sasa ni wazi chini ya anko .....upinzani unakamuliwa kila kona kwa jina la hapa kazi tu na demokrasia style mpya au style ya zama zile - hati tuliitaga one party democracy. Tusiposema leo kuna siku tutajikuta tuko pekeyetu.
 
Sasa ni wazi chini ya anko .....upinzani unakamuliwa kila kona kwa jina la hapa kazi tu na demokrasia style mpya au style ya zama zile - hati tuliitaga one party democracy. Tusiposema leo kuna siku tutajikuta tuko pekeyetu.
Watu wafanye kazi, siyo muda wa kusimama majukwaa.
 
Narudia mara kwa mara,naombeni mniombee,nitawatengenezea hii barabara,nasikiliza sana mahubiri yako
 
Back
Top Bottom