Viongozi CCM na Jumuiya zake: 'Zungumzeni Mambo Yanayohusu Maendeleo Ya Wananchi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi CCM na Jumuiya zake: 'Zungumzeni Mambo Yanayohusu Maendeleo Ya Wananchi'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SHIEKA, May 11, 2012.

 1. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,129
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Habari zenu WanaJF
  Hizi dukuduku nimeziweka moyoni mwangu muda mrefu sasa. Tangu kuahirishwa kwa mkutano wa Bunge tarehe 23/4/2012, na kuibuliwa kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, vichwa vya viongozi wengi wa ccm vilipata kizunguzungu na kushindwa kabisa kuwaambia wananchi ukweli wa hali ya uadilifu wa wale waliokabidhiwa madaraka. Mabilioni ya hela yameibiwa ilhali wananchi wengi hawana maji safi ya kunywa; watoto hawana madarasa ya kusomea,na dawa hakuna hospitalini. Badala ya viongozi wa ccm kwenda kwa wananchi na kueleza ni hatua gani muhimu za kuwachukulia hawa wezi, viongozi wanaweka nguvu nyingi kuwaponda wapinzani. Na hasa baadaya mkutano wa chadema kule Arusha tarehe 5/5/2012, ndo kabisaa ccm imepoteza mwelekeo. Sasa hivi wanachojua ccm ni kauli ya Mh. J Nassari. Kauli ya mbunge huyu wa chadema imegeuzwa kuwa ilani ya ccm.

  Mwenyekiti wa UVCCM taifa Mh M. Shigella kaenda Manyoni na kuhutubia wananchi na mojawapo ya agenda ni kauli ya Nassari. Watu wanakabiliwa na matatizo mengi ya maendeleo halafu unasimama na kuwaeleza eti mtu mmoja kule Arusha aitwaye Joshua Nassar kasema kaskazini watajitenga, itawasaidia nini watu wa Manyoni? Kwa nini usiwaeleze jinsi watakavyofaidi chenji ya rada iliyoletwa hivi karibuni?

  CCM wallahi mnashangaza na kuaibisha! Elezeni utekelezaji wa ilani yenu ya uchaguzi mliyoipamba sana mwaka 2010 na muache kugeuza Nassari kuwa ilani yenu.

  MUNGU AWASAIDIE
   
Loading...