Katika mkoa wa Iringa watu wa daladala wana vioja sana. Sio ajabu dereva kushuka kwenda kusalimia rafiki zake. Daladala inasimama kituoni mpaka daladala nyingine iwe inakuja. Konda anamwambia dereva wakashushe abiria ili wawahi pombe. Wanawajua abiria wao, utasikia chukua yule mzee anashuka semtema. Kila abiria anataka ashushwe anapotaka hata kama ni karibu karibu. Utawasikia shusha hapo kwenye mchongoma, au shusha hapo sheli (kilabu cha ulanzi). Yani kuna vioja vingi. Mliowahi kufika Iringa mnaweza kuongezea.