Landed Property
Member
- Nov 17, 2011
- 40
- 7
Ndugu wanaJF
Vipo viwanja sabini vyenye ukubwa wa sqm 700, 900, 1200 eneo liitwalo Kwembe. Ni 3km kamili kutoka morogoro road upande wa kushoto kama unatokea DSM. Viwanja vimegawanywa na mmiliki wa eneo kwa kuweka barabara za kutosha, havina hati ya wizara ila ni halali kwa makazi. Bei ni kuanzia shs 4m. Ukipenda na uwezo unaruhusu unaweza kuviunganisha hata vinne sehemu moja.
NOTE; mimi sio muuzaji wala dalali ila ni mkazi wa jirani na eneo hilo hivyo nimeamua kuwashirikisha ili kuwasaidia wanaohitaji.
Asante
Yeah!Wanajamvi kuwekeza katika ardhi ni muhimu sana lakini chukueni tahadhari kubwa eneo hilo lina mgogoro sana na pia kuna kesi mahakamani
Google ardhi Kwembe halafu soma kwenye link: Mgogoro wa Kwembe watua kwa Pinda - Bwagamoyo
Sisemi kila eneo Kwembe lahusika lakini km alizotaja toka Moro road likpo kwenye mradi
Wanajamvi kuwekeza katika ardhi ni muhimu sana lakini chukueni tahadhari kubwa eneo hilo lina mgogoro sana na pia kuna kesi mahakamani
Google ardhi Kwembe halafu soma kwenye link: Mgogoro wa Kwembe watua kwa Pinda - Bwagamoyo
Sisemi kila eneo Kwembe lahusika lakini km alizotaja toka Moro road likpo kwenye mradi
Asante mkuu, ila kuna
PAGALE; lenye ramani ya kisasa (1masterroom, 2beding room, 1 seating room, 1 dinning room, smallstore and a public toilet)
LOCATION; kunduchi mtongani( njia panda ya wet n world), ni ya pili kutoka barabarani
BEI;25mil(haina dalali)
CONTACTS; 0714 581449(Joshua)
"KARIBUNI NYOTE"
Nijuacho ni kwamba Kwembe kuna migogoro ya ardhi, labda kama mgogoro umeisha. Binafsi nilikuwa na kijieneo changu huko na nafahamu kilichokuwepo huko.
Mgibeon
Unaweza kunielimisha Pagale ni nini? Msingi wa nyumba ulioanzwa or nini ? Na Pia ukubwa wa kiwanja je? picha if possible pls!
Kwa taarifa za jana toka kwa dalali mmojawapo (Shabani) wa viwanja hivyo na mimi mwenyewe nilifika hapo kwenye viwanja;
Vimenunuliwa zaidi ya 50% tayari na jumamosi walionunua walikuwa wanajengea mipaka vizuri.
I wish ofisi za ardhi zingewashawishi watu wenye maeneo wanayouza (ambayo hayajapimwa) wafanye kama huyu bwana alivyofanya ---- yaani amevigawa viwanja vizuri, amechonga barabara zenye upana wa kutosha.... nimesikia alishirikiana na afisa ardhi/mpimaji wa ardhi mmoja (tetesi) kuvigawanya. Hakika eneo kama hili sitegemei kuona mwonekano kama wa baadhi ya maeneo ya uswahilini ambapo hata kiwanja cha sqm 100, 80, 150 unapata kisha hata mkokoteni hauna njia.
Karibuni Kwembe tujenge mtaa wetu
Kama vipo upande wa kulia sambamba na Maduka sita (kama unatoka Serikali ya Mtaa kwenda mjini) basi vipo salama lakini upande wa kushoto ogopa sana kwani kuna mgogoro mkubwa pale kwani watu wa ardhi wlipima eneo hilo kihuni wakiwalipa watu wa kudadikika na hivyo kupelekea mgogoro. Pia kuna kiwanja cha Kanisa la SDA wao wana ekari kama 22 hivi hivyo ukiingia kichwa kichwa wale ni Radical sana watakuondoa tu.
Upande wa kushoto ni salama mwenyewe ni Afisa Ardhi wakati wa mradi alipakwepa makusudi kwa nia labda ya kuuza baadaye kama ni yeye anauza Okay nunueni kwani ni kwake (Yaani pale kwenye container la celtel)
Mimi nakaa maeneo hayo na nimeshuudia watu wakiuziwa migogoro kwa bei kubwa sana
Bwana Nyati,
asante kwa kutoa taarifa zaidi.
mimi Binafsi baada ya kusoma post ya kwanza jumamosi nilifika eneo husika.
1. Nimeonyeshwa eneo linalouzwa - lipo upande wa kulia baada ya maduka sita kama unaenda serikali ya mtaa kutokea mjini.
2. Ni eneo linalopakana na eneo lililopimwa la mradi (Block A kwembe).
3. Eneo linapakana na eneo la Kanisa SDA (upande wa Kusini), wamiliki wengine pande za Magharibi na Kaskazini, Barabara kubwa ya Kwembe (Mashariki).
Ni kweli eneo linasemekana halina mgogoro na baada ya kuwasiliana na rafiki yangu from ministry of Lands amenieleza kuwa eneo hilo lilipimwa zamani sana kama shamba ila halitambuliki tena kama limepimwa hivyo lipo free kwa yeyote kujipimia akipenda ila ni kwa ajili ya makazi.
Kwa kusikia hivyo nilijikuta nashawishika kununua na asubuhi ya leo nilitoroka kwa mwajiri na hapa nimetoka kulipia viwanja viwili - sqm 1200 @ Shilings 7.5m.
Ndg Nyati,HONGERA SANA na KARIBU KWEMBE. Katika maelezo yako umejiridhisha kuwa angalau kwa asilimia 99.99999% hata mimi sina maswali zaidi hapo ila juu ya hiyo Block A, ni ya mradi upi? kwani mradi wenye mgogoro una blocks nne (Kitalu 1 hadi 4) Block 1 ni karibu na shule ya Babro Johansen, Block 2 ni karibu na Container kwa itandula, Block 3 ni maeneo ya Maduka matatu, Block 4 ni pale kulia kwa Maduka sita. Hivyo labda lipo jirani na Block 4.
Pia kuna barabara ya mita 70 kwenda kwenye mradi wa Muhimbili
Hata hivyo karibu sana, nitaanzisha vikao vya wan JF Kwembe, Kibamba na Luguruni pale La Paz hivi karibuni. By the way wengine wajue kuwa karibu na hapo kutakuwa na mradi wa Chuo kikuu cha Muhimbili, Chuo cha St Joseph na mji wa mfano wa Luguni hivyo eneo linapanda value haraka sana