mara nyingi mzani mmoja hautambui risiti za mzani mwingine. na siku zote wanajaribu kutengeneza mazingira ya kudoubt ukweli wa mtoa risiti kuwa mnaweza kuwa mmeweka mzigo mwingine btn mizani, ambacho sio kweli kabisa. kuhusu kuchukua hatua za kisheria, hapo ndo uswahili wetu unapoingia. mara nyingi hiyuo process inachukua muda sana na while unachukua hatua hiyo gari lako utaliacha mizani? mwishoni kwa sababu wewe ndo mnyonge na unataka uachane na hiyo kadhia unaishia aidha kulipa faini uliyopewa au kutoa kitu kidogo yaishe na ww uendelee na shughuli zako.[/QUOT
Mi nitapingana na wewe hadi mwisho mkuu kwani nina uzoefu mkubwa ktk mambo ya mizani ndo maana napinga, hawa watu huwa hawaamini risiti za mizani ya nyuma kwa sbb,
1: kuna magari huongeza mafuta njiani
2:Baadhi ya madereva huwa wanaongeza mizigo njiani bila kujari gari lake lilikuwa na uzito kiasi gani na huingia mizani kupima bila kujaribu kupima hata mizani ya kujaribia kuona baada ya kuongeza mizigo uzito uko vip?
3:Kuna baadhi ya mizigo kama sukari, chumvi, cement na box ambayo inaweza kuhama axle moja kusogea axle nyingine pale ambapo dreva atapinga matuta bila kujari au kupita barabara mbaya zenye mashimo n.k na kuingia mizani bila kuangalia kama mzigo umesogea au vip
lazima tu tukubali kwani hiyo ni mizigo na mifuko inateleza uwezekano wa kusogea ni mkubwa
Mwisho naomba tusiwalaumu watu wa mizani wao kweli wanaweza wakawa wanachukua kitu kidogo ila si kwa kumonea mtu pasipo na gari lake kuwa na tatizo