Hizi ofisi zetu zina vikao sijapata ona. Yaani kila ofisi ukijaribu kuweka appointment kumwona mtu fulani, utasikia yupo kwenye kikao tangia asubuhi. Ukisema uje kumwona kesho, utasikia kuwa atakuwa kwenye kikao pia
na keshokutwa
.na mtondogoo
wiki mzima.
Ni hili sio suala la ofisi moja tu. Ukijaribu kukutana na wahusika wako katika ofisi tano tofauti kwa siku, basi nakuhakikishia kuwa wanne watakuwa/utaambiwa kuwa wako kwenye vikao.
Swali la kujiuliza ni je watanzania wanafanya Kazi saa ngapi, ikiwa kama wanatumia muda wao mwingi kwenye vikao? Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa kila jumatatu na jumatano huwa wanavikao karibu siku mzima. Saa 3 asubuhi wanakikao mpka saa 6 mchana. Wanatoka wanaenda lunch, halafu wana kikao kingine kunanzia saa 8 mpaka saa 10 jioni. Baada ya hapo wanazugazuga kwa lisaa hivi, halafu hao wanachumpa. Siku imeisha. Sasa ukiangalia utaona kuwa, kati ya masaa 40 ya kazi ya wiki mzima, ndugu zetu hawa wanapoteza masaa 16 ya jumatatu na jumatano kwenye vikao. Ina maana wanabakiwa na masaa 24 tu. Na ukitoa muda wa kusoma magazeti, kupiga umbeya, kwenda kununua vocha za simu, kutembelewa na marafiki makazini, n.k
basi utaona kuwa hata hayo masaa 24 yaliyobaki yanautata kwenye kupiga mzigo.
Nikijaribu kuchambua pengine sababu inayofanya vikao vipewe kipaumbele maofisini, nitakuja na yafuatavyo (hamna mtiririko maalum):
Maamuzi ya pamoja (jumla)
Huu mlolongo wa vikao visivyoisha unaweza kuashiria kuwa watanzani ni waoga kufanya maamuzi wenyewe (Individual Decision Making). Badala yake tunapendelea kufanya maamuzi ya pamoja (Collective Decision Making). Kwa nini tunapenda maamuzi ya pamoja? Kwa sababu iwapo mambo yatakwenda tofauti na mategemeo, basi hakuna wa kubeba mzigo wa lawama. Kisingizio kitakuwa ni si tulijadiliana na kufanya maamuzi wote pamoja. Hatupendi/tunaogopa ku-take responsibilities.
Sitting Allowances
Hili linajulikana kwa upana zaidi. Limeshajadiliwa kwa mapana zaidi katika mada mbalimbali.
Kuna dada mmoja anafanya kazi kwenye NGO moja hivi ya wazungu inayoshughulika na ishu za uzazi wa mpango na utokomezaji wa magonjwa ya muda mrefu (malaria & co.) katika nchi za duni ya tatu. Sasa siku moja waliandaa kongamano la kujadili jinsi ya kutokomeza/kupunguza magonjwa hayo. Basi wakatuma mialiko kwa wizara ya afya, mahospitalini, na wahusika wa jiji. Unajua nini? Waalikwa wote walitaka wapewe sitting allowances kwenye kongamano linalohusu shughuli ambazo ni sehemu ya kazi zao. Wazungu wakasema get the f*@$ outta here.
Tu wavivu
Vikao hivi vinaweza pia kuashiria kuwa sisi ni wavivu, tusiopenda kuchapa kazi. Badala yake tupendelea kukusanyika na kupiga soga huku tukisingizia kuwa ni tunajadiliana mambo muhimu ya kiofisi. Unaweza kukuta humo ndani kwenye conference room muda mwingi unatumiwa kwa mabishano na majigambo baina ya wapenzi wa Manchester United, Arsenal na Chelsea, wakati wapenzi wa Liverpool wakigwaya kimya. Au pengine muda mwingi utatumiwa kumzungumzia migogoro ya kisiasa, vituko vya fataki, mambo ya EATV na Ze Comedy yao mpya, na bar zinazopika kitimoto kinono zaidi.
Yaani iliradi siku inaisha bila kufungua faili lolote lile.
Hatupendi Ugeni (wa kiofisi)
Je tunavyoambiwa kuwa fulani yuko kwenye kikao ni kweli? Au pengine huyo fulani amehamua kujifungia ofisini (hope anachapa kazi) na kumwambia administrative assistant wake kuwa watu wote (isipokuwa x, y, na z) wajao kumuona waambie kuwa yuko kikaoni? sidhani kama jibu la swali hili laweza kuaptikana.
Oh well, sababu zinaweza kuwa nyingi, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa wingi wa vikao hivi hausaidii ufaninisi wa uchapa kazi kama managements zinavyotaka kuamini. Ni upotezaji wa muda, ambao matokeo yake ni ushindwaji wa ufikiaji wa malengo na maazimio.