Vijue vipaumbele na sera za ndugu Juma S. Mtoro, mgombea nafasi ya mwenyekiti UVCCM taifa

Nyasa Girl

Member
Jul 11, 2017
10
19
VIJUE VIPAUMBELE NA SERA ZA NDUGU JUMA S. MTORO, MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI UVCCM –TAIFA.

TAARIFA MAHUSUSI

Jina: JUMA SEIF MTORO

Kuzaliwa: 1987.

Mkoa: Pwani.

Wilaya: Bagamoyo


ELIMU

Chuo Kikuu Cha Dodoma-Shahada Ya Kwanza Ya Maliasili,Utalii na Urithi wa Utamaduni.



UZOEFU KATIKA UONGOZI

►2009-2012: -Katibu tawi la West Kinangali-UVCCM, Dodoma Mjini.

►2009-2012:-Mjumbe kamati ya Utekelezaji UVCCM kata ya Chamwino.

►2009-2012: -Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UVCCM wilaya ya Dodoma Mjini

►2009-2012:-Mjumbe Wa Mkutano mkuu UVCCM Mkoa wa Dodoma.

►2010:-Kaimu katibu UVCCM Wilaya ya Dodoma Mjini.

►2010-2012: - Mjumbe wa Halmashauri kuu tawi la Chuo Kikuu Dodoma.

►2010-2012: -Mbunge wa bunge la Serikali ya Wanafunzi chuo kikuu Dodoma.


SHUGHULI ZA KIJAMII NJE YA CHAMA

►2013-2014.Mratibu mradi wa elimu ya katiba kwa vijana Tanzania.

►2013-2015.Afisa Mahusiano wa vijana Shirika la Restless Development Tanzania

►2014-2016.Mkufunzi elimu ya ubora na ufanisi makazini kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania .

►2015 hadi Sasa:-Mtafiti na Mshauri mkuu kituo cha Redio E-Fm na Tv-E Tanzania.

►2016-hadi sasa .Mkurugenzi Mtendaji wa Mtoro education Foundation Tanzania.

Vipaumbele;

►Kutengeneza Mitaji Na Ajira Kwa Vijana Kupitia Mashamba ya Jumuiya na Serikali.

-Kuanzishwa kwa mashamba ya Miwa, Mgulazi ,Mbigiri,Kagera na kilombero kulima Ekari 200 kila sehemu na kuuziwa viwanda.

-Kilimo cha Kisasa cha umwagiliaji na vitalu nyumba (Greenhouse).

-Pia uanzishwaji wa vituo maalum kila mkoa ,ambapo zitajengwa greenhouse kwa ajili ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana na kuwezeshwa kimitaji kupitia vikundi.

–Kuanzisha viwanda vidogo vya usindikaji mazao na kuongeza thamani.

►Kubuni Vyanzo Vipya vya Mapato.

-Vyanzo Vipya vya Mapato vitabuniwa kutokana na jiografia ya eneo husika , na fursa zilizopo nchini ili kuifanya Jumuiya ikue kiuchumi na kujiendesha kitaasisi.

-Kuanzishwa kwa kilimo cha kisasa katika kila wilaya na mkoa ,Kubuni Vyanzo vya Mapato kutokana na fursa zilizopo wilaya husika , mfano Gairo –viazi vitamu ambavyo vina soko kubwa nje ya nchi sababu ni vya asili n.k

►Kuifanya Uvccm Taifa Kuwa Ya Kisasa.

-Jumuiya iwe kimbilio la vijana mbalimbali nchini , kupambana kurudisha kata na majimbo yaliyo upinzani , kutoa semina, makambi na madarasa ya itikadi mara kwa mara kuhusu chama na Jumuiya katika kukipigania chama na kutekeleza ilani ya chama kupitia Kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.

►Kuifanya Jumuiya Ijiendeshe Kwa Miradi Iliyopo

-Jumuiya ikiwa imara kiuchumi , tunatengeneza taasisi imara ya vijana watakaoweza simamia serikali ,hivyo miradi ya sasa yenye harufu ya ufisadi tutaipitia upya na wawekezaji wote ili miradi iwanufaishe vijana na Jumuiya, hii itapunguza Jumuiya kuwa ombaomba hasa wilayani na mikoani wakati wa chaguzi za Jumuiya na shughuli mbalimbali.

-Viwanja vilivyopo wilayani na mikoani kutafuta wawekezaji kwa kuingia ubia na wawekezaji ili Jumuiya inufaike , mfano mvomero kutumia kiwanja chao kilichopo wami Sokoine , kukiendeleza kwa kushirikiana na mwekezaji na Viwanja vya maeneo mbalimbali Tanzania.

-Pesa inayopatikana , katika miradi ya wilaya , itatengwa baadhi na kutoa posho kwa makatibu wa Jumuiya kata , walipwe posho ya kuanzia 5000 kuwapa motisha ya kufanya kazi na hali itakavyokuwa inatengemaa posho itakuwa inapenda.

Maslahi ya watendaji wa Jumuiya.

Kuboresha maslahi ya watendaji wa Jumuiya kuanzia ngazi ya Taifa hadi wilayani , kwa kufanya yafuatayo;

-kuingia makubaliano na taasisi za kifedha zianze kuwakopesha

-kuingia makubaliano ya watendaji kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii

-kuboresha mazingira ya kiutendaji kwa kupeleka samani na vifaa vya kufanyia kazi ,kama printer , kompyuta n.k

-kuwezesha watendaji wapate Usafiri kwa mkoa gari ya Jumuiya na wilaya pikipiki Zitakazo saidia shughuli za Jumuiya.

-kurekebisha mishahara Iendane na hali ya maisha ya sasa.

►Kupigania 5% (Asilimia tano) ya mfuko wa vijana kila wilaya ili iwasaidie katika ujasiliamali.

Vijana kila kata , watasaidiwa kuanzisha vikundi vya vijana na kufanya ujasiliamali kupitia pesa za 5% na hii itasaidia vijana kupambana na tatizo la ajira , kwani vikundi hivyo vitaunda saccoss ya wilaya na saccoss za wilaya zitaunda saccos ya mkoa.


Misingi ya Kutekeleza Majukumu yangu;

-uadilifu
-uwazi
-uaminifu
-kujali usawa

Kauli Mbiu: RASILIMALI ZA JUMUIYA ZITENGENEZE AJIRA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom