Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Hapa chini nitaeleza baadhi ya vijimambo vya wanawake vinavyodhibitisha udhaifu wao wa kutokuwa wakweli:
(1) Tangu kukua kwangu nimewahi kutembea na mwanaume mmoja tu maishani mwangu tena alinibaka na kunitoa bikra bila ridhaa yangu- Labda tu niwashauri wanaume waachane na hili jambo la kutaka kujua mwanamke anayemtongoza au aliye na uhusiano naye aliwahi kuwa na mahusiano na wanaume wangapi, atadanganywa tu.
(2) Yaani mpenzi wangu nime enjoy sana siku ya leo, kwa mara ya kwanza nimefika kileleni, wewe ni hodari kweli – Mh, labda kama kweli umepiga game la kufa mtu, lakini kama ulipiga famba, basi hapo jua amekutukana sana kimoyomoyo huku akikusanifu kwa maneno ya ulaghai ili ujione kidume lakini wapi atakudharau sana
(3)Mimi sijawahi kuwa na mahusianao na wanaume wawili kwa wakati mmoja katika maisha yangu na sijawahi kukusaliti hata mara moja – Kwa wanawake mara nyingi kama yuko kwenye uhusiano ambao haujaota mizizi, lazima kutakuwa na zombie limewekwa kiporo ili mambo yasipokuwa mazuri ana pa kukimbilia, hapa ndipo ulipoibuka ule msemo wa kiingereza usemao friend with benefit au friend zone.
(4) Nitakuwa tayari dakika sifuri tu- Ha ha ha ha haaaaa thubutu, hapo jiweke tayari kusubiri kwa muda wa saa nzima, wanawake hawajui kutunza muda hilo linajulikana na hata wao wenyewe wanajua kuhusu jambo hilo. Waje hapa wabishe……..
(5) Sawa yameisha bwana – Mh! Kama umemkosea mwanamke ambaye una uhusiano naye halafu unapoanza kumuomba radhi kwa kujieleza akakwambia hivyo, Mai weeee, jua hapo anamaanisha atakuonyesha cha mtema kuni, jaribu kutafuta suluhu kupitia kwa ndugu zake au watu wake wa karibu anaoheshimiana nao ili uwe na uhakika kama yamekwisha kweli, la sivyo……. Fill the blank space yourself.
(7) Kwa kawaida huwa sitoi namba yangu ya simu hovyo kwa wanaume, lakini sijui kwa nini nimekuamini na kukupa namba yangu kirahisi hivi – Kama unataka kujua ukweli kwamba aliwahi kuwapa namba yake ya simu wanaume wangapi, basi kwa taarifa yako wewe utakuwa ni mwanaume wa 9,999 kukupa namba yake ya simu. Kwa hiyo usijione kama ni mwenye bahati, thubutuuu….
(8)Ndiyo kwanza nimetimiza miaka 24 – Hapa ongeza mingine mitano kupata umri sahihi
(9)Wewe ni mwanaume wenye moyo wa upendo sijapata kuona –Hapa jiulize mara mbili, maana kwa mwanamke kukuona una upendo wakati mwingine ni vile anavyokupelekesha na wewe unajiendea tu kama zezeta
(10)Sihitaji kuwa na mahusiano na mwanaume kwa sasa- kauli hii hutolewa na wanawake walioumizwa kimapenzi, hivyo wanaogopa kuumizwa tena