Vijana wapenda CHADEMA tafadhali msije mkayafanya haya!

Dnashon

Member
Feb 19, 2016
58
33
Ndugu zangu wapenda haki na demokrasia ya kweli nidhahili pasipo shaka Serikali imekuwa ikotoa matamko kupitia viongozi wake WA ngazi mbalimbali, baadhi ya kauli zimekuwa zikitafasiliwa wazi kuwa zinakandamiza Uhuru wa siasa za vyama vingi hasa vyama pinzani.
Bila kumumunya maneno jeshi la polisi halioneshi dhamira ya dhati ya kiutendaji bila kuegamia upande wowote! Hii Ni hatari Sana kwa kesho ya taifa letu.
Vijana wenzangu, watanzania wenzangu...tarehe 23 July...itakuwa siku ya majonzi kwa wengi kama kweli mtadiriki kwenda Dodoma kuzuia mkutano wa CCM.. vijana watapoteza maisha na wengine wengi kuumia na kutiwa ndani bila dhamana. Polisi kwa namna yote ile hawatasita kufanya lolote kuilinda serikali na Chama ambawo kiasi kikubwa Watakuwa DODOMA.
Kabla ya kufikia huko, hatuna budi kukaa na kutafakali kwakina njia bora ya kufanya. Maisha yapo baada ya tarehe 23.
Wengi watasema haki gharama yake Ni kubwa hata kifo, Ni sawa lakini bado tunahitaji mikakati dhabiti ambayo italeta mapinduzi makuwa ya kiutawala katika taaifa letu. Hakuna mzazi ambae Yuko tayari kumzika mwanae kisa mkutano wa CCM.
 
Mkuu usiwe na hofu,Bavicha wamesitisha kwenda Dodoma baada ya Polisi kutoa ufafanuzi kwamba mikutano yote ya ndani kwa vyama vyote imeruhusiwa.Ikumbukwe Bavicha waliamua kwenda Dodoma kuzuia mkutano wa ccm baada ya Polisi kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani na kuruhusu ile ya CCM.
 
Back
Top Bottom