Vijana wangu wametapeliwa kambini

SR senior

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
358
68
Nina vijana wangu wanaonisaidia katk kujikwamua kiuchumi, walipigiwa cm na matapeli wakihitaj mzigo wa turubai thelathin walipokutana mtu mmoja wa makamo aliwalaghai kua anaenda kuziuza jeshini kwa ajili ya wahanga wa mafuriko.. Akawatolesha photocopy kitambulisho kisha wakaingia kwenye teksi kuelekea kambi ya jeshi pale taifa.. Walipofika pale wakawaambia washuke getini wao wanatoka muda c mrefu.. Hawakutoka au walitokea get la uhasib, cna hakika... Tulipokwenda ripot chang'ombe wakasema matukio ya hapo yamekithiri na yawezekana wanajeshi wanahusika, they had no option zaid ya kushauri labda turushe kwenye mitandao.. Nmesikitika sana kama kwel kuna uhusiano wowote na uhusika wa wanajesh kwenye hili cio uadilifu ht kdg tena kumdhulumu mmachinga anayetafuta jua lote mwilini ni laana kubwa..
 
Kaa chonjo mjini, popote pale usikubali mtu aondoke na Mali yako bila kuacha dhamana, ila unapoiuzia taasisi bidha sidhani Kama wananunua kwa mtindo huo. Kuna wajanja hutumia maeneo wanayoyafahamu pa kupenya kutapelia watu. Hao wala sio wanajeshi, ni wenye kazi ya wako wengi kila kona hapa Dar, nenda kwenye maduka ya kubadirishia pesa wapo. Cha msingi hapa mjini kila ufanyalo jua wenzio wameshatangulia, hivyo kuwa makini. Ila sehemu husika msiruhusu watu wasio na mpangilio kuzurura maeneo yenu ona mnapakwa mavi.
 
Duh pole sana, hivi hakuna CCTV? Huwa haziongopi kabisa zile aiseee

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
 
Hao ni matapeli tu na Wanajeshi hawahusiki kwa lolote hapo. Kuna jamaa yangu walijaribu kumtapeli water pump za M30 sema akawastukia mapema. Hawana uhusiano na jeshi sema wanajua wakitaja jeshi ni rahisi watu kuamini.

Duc in Altum
 
Kuna Mzee Wang mmoja ye katapeliwa magodoro ya milioni Tisa na nusu, walikubaliana na tapeli kwamba atamlipa kwa cheque, so yule tapeli akapeleka cheque bank ikapokelewa akapewa copy ya slip akairudisha dukan, mzee akaamin akatoa mzigo, baada ya siku moja cheque ika-bounce kumbe akaunti ya ile cheque ilishafungwa siku nyingi, Mzee hajui kwa kumpata yule jamaa na hakuwahi kufanya nae biashara ndo Mara ya kwanza. So tuwe makini jaman mjini shule
 
Back
Top Bottom