bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,015
- 4,982
Katika hali isiyo ya kawaida katika nchi yetu, mapinduzi ya aina yake yametokea kutokana Na ukosefu mkubwa wa ajira , vijana wengi wasomi wamegeuka kuwa Machinga wa kutembeza bidhaa mbali mbali mitaani ikiwamo nguo za mitumba, Viatu, pamoja Na kufungua vibanda vidogodogo vya biashara kutokana Na kukosa mitaji ya kufungua biashara nyingine.
Kwa upande mwingine wengi pia wamegeukia kilimo licha ya changamoto nyingi wanazokutana nazo huko, wengine wamegeuka kuwa matapeli, lakini kubwa zaidi ya yote vijana wanalalamika kuwa kipindi hiki Ni kigumu kuliko kipindi chochote walichowahi pitia katika maisha yao kutokana Na hali ngumu ya uchumi wa sasa.
Mh. Magufuli fanya jambo basi kuokoa kizazi hiki. Juzi ndoa ya jirani yangu hapa imevunjika kutokana Na hali ngumu ya maisha, kila mtu kaelekea alikotoka