kuna ombwe kubwa sana katika fani ya uandishi katika makala na maandiko mengine kwa baadhi ya magazeti! Katika historia ya binadamu tangu zama za kufikiri na kukua kwa fikra au age of enlightment hakuna hoja isiyo na mlengo au itikadi hata kama mtoa hoja binafsi atajitaidi kuonyesha yeye si wa mlengo huu au ule, wasikilizaji au wapokeaji wa hoja wataziona hoja hizo ni za mlengo au itikadi fulani!!! Kwa hiyo jambo la muhimu si kuwa katika chama hiki au kile jambo la msingi ni kuwa na hoja zenye utaifa pasipo kuteteleka na hiyo ndiyo itikadi ya kweli! Kuhusu vijana kulishwa hoja si jambo geni katika dunia , ni jambo la kihistoria na ndiyo lilizaa uhuru,mabadiliko na maendeleo ya dunia na ndiyo sababu tukawa na kina Nyerere, Nkruma, patrice Lumumba, Mandela, Stivene Biko n.k. Kwa hiyo katika jamii wanakuwa chazo cha fikra pevu na wengine ni kuzipokea na kuzitenda kwa namna walivyozielewa! Kwa hiyo tatizo la msingi ni kupima hoja, namna na wakati wa kuzitenda! Kundi la vijana ndiyo lenye kiu kubwa ya mabadiliko, maendeleo na ndoto za kuona taifa lenye usawa na haki kwa watu! ndilo kundi lenye changamoto nyingi za maisha na kutafakari kina hatma ya kesho! Hivyo ni vizuri sera zote za maendeleo zikagusa vijana kwa uhalisia na vitendo na si maandiko tu!