Vijana tunaomba umri wa kustaafu uwe miaka 45 hiari na 55 lazima

kutakuwa na wizi sana serikalini! na pia mifuko ya pension itakufa maana utamlipa mtu miaka mingi mpaka uzee wake! waliocalculate ni waliosoma cuba
 
Hizi ni kama akili za panya. Badala ya kutaka matatizo ya upatikana ajira yapatiwe ufumbuzi wewe unataka kuhamisha kutoka kwa vijana kwenda kwa umri wa kati. Tanzania elimu yetu inatufanya tusitafakari kidogo. Tatizo la ajira linatokana na uongozi mbovu wa CCM na siyo muda wa kustaafu.
 
kutakuwa na wizi sana serikalini! na pia mifuko ya pension itakufa maana utamlipa mtu miaka mingi mpaka uzee wake! waliocalculate ni waliosoma cuba
Hiyo ndio fikra potofu waliyo nayo baadhi ya watendaji wetu, hilo linaweza kufanyiwa utaratibu mwengine tofauti na huo wa zamani.
 
Mifuko ya pension haina pesa, fatilia ulaya wanataka iwe 70. France maandamano yalikua mengi kupinga 65.

Tatizo ni mifuko ya pension haina hela kulipa ukistaafu mapema.
 
Vijana hawa waimba singeli
 
Sasa wewe umeenda nje ya Mada.
Hapa sizungumzii tatizo la ajira bali nazungumzia jambo mojawapo linalo wazuia vijana wengi kuajiriwa serikali moja wapo ni umri wa kustaafu, hivyo nimependekeza upunguzwe uwe kuanzia miaka 45, itasaidia vijana kupata nafasi.
 
Ama kweli kua uyaone. Huzungumzii tatizo la ajira bali unapendekeza umri wa kustaafu uwe 45 ili vijana kupata nafasi!!!! Nilikuwa najua kuwa tuna tatizo la elimu ya kukariri lakini sikujua kuwa tatizo ni kubwa kiasi hiki!!
 
Reactions: FWC
Viajana hawa hawa wa kataa ndoa?
Wanataka kuoa wakiwa 55, sasa wataowaje wakishastaaf?
 
Lengo ni kutumikia au kupata kipato. Funguka mleta mada.
 
Mtu mwenye miaka 45 kama sio bonge na hali hovyo mbona bado ni kijana mbichi sana?

Afu ukute alipata ajira serikalini akiwa na 35. Yan 10yrs ya kula mshahara bado haijamtosha unataka astaafu?
 
Hao vijana wenyewe weledi kazini sh wazee uzoefu wanatekeleza majukumu yao safi kwa wakati wakiwa kazini wanajua wajibu wao na sio kuchezea simu muda wa kazi na kuchimbua page za udaku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…