musa ndile
Senior Member
- May 6, 2011
- 105
- 34
Kwa muda mrefu sana tangu harakati za kisiasa zilipoanza nchini sikuwahi kupata fursa ya kuingia kwenye mitandao mbalimbali hasa jamii forum ambayo nilikuwa mdau mzuri sana, nashukuru nimerejea lakini kwa masikitiko makubwa nimekuta jamii forum ya Leo ni tofauti sana na jamii forum niliyoijua awali, miaka kadhaa iliyopita kweli jamii forum ulikuwa ni mtandao makini wenye watu makini na hata hoja zilizokuwa zinajadiliwa zilikiwa ni zenye mashiko na umakini wa hali ya juu lakini nasikitika sana kuona Leo hii vijana wenzangu tena wasomi wanajadili humu ndani Umbea, majungu na Mipasho hii ni hatari sana kwa afya na ustawi wa Taifa letu, nimeingia Mara nikapata shida sana na kuanza kujiuliza hivi hakuna mambo ya msingi ambayo tungeweza kujadili ili kuleta tija kwa Taifa letu??? Ushabiki wa kisiasa umefanya baadhi ya vijana wawe vipofu si CCM tu kama tulivyowazoea lakini hata vyama vya upinzani. Ni muhimu sana tujue kufanya a GOOD CRITICAL ANALYSIS kabla ya kufanya argument la sivyo safari yetu itaendelea kuwa ngumu sana tens isiyo na future this is very danger. BETTER THINK AND UNITE" By J.K.Nyerere.