Vijana Tuichukue Nchi Yetu 2014-2015

Vijana Tuichukue Nchi Yetu 2014-2015

ibange

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,543
Reaction score
553
Vijana wote tuungane katika hili, tuweke tofauti zetu pembeni. Tuanze kujiandaa ili mwaka kesho tushike serikali za mitaa,2015 tukamate Ikulu. Ni mapinduzi yasiyomwaga damu, silaha yetu ni kujiandikisha, piga kampeni, piga kura, linda kura, linda ushindi.
 
Hapo umeongea tunahitaji CCM Mpya!

Mfumo uliopo wa 'SIASA NI AJIRA/BIASHARA' hauruhusu vijana wa kweli kushika hatamu za nchi. Hivyo vijana waamke kwanza kubadili mfumo unaowafanya vijana kutumika kama wapambe, unaowabana wale unaowaongelea, wanaoweza kuiletea nchi yao na watu wake MABADILIKO ya kweli.
 
Kwani vijana wengi mpo chana gani? Ama mnataka uchukua nchi kupitia mgombea binafsi? Haya jipangeni vizuri.
 
Chama cha vijana ni kama gari tu la kutuvusha. CCM haiwezi kutuvusha ni gari mfu, CUF haina vision inatetea zaidi Znz. Kwa maoni yangu chadema linaweza kuwa gari muafaka, lituvushe tu mambo mengine baadae
 
Acha ujuha wazazi wako wamekuzaa leo unajidai unainchi hizi akili mbaya sijui mnazitoa wapi vijana wa bavicha.
 
Chama cha vijana ni kama gari tu la kutuvusha. CCM haiwezi kutuvusha ni gari mfu, CUF haina vision inatetea zaidi Znz. Kwa maoni yangu chadema linaweza kuwa gari muafaka, lituvushe tu mambo mengine baadae
Hapo ulipo jibanza mbona peupe sana mgogo upo nje unaonekana utaaibika bure.
 
Frankly speaking linapokuja suala la vijana kwenye nafasi kubwa za uongozi najiuliza mara mbili mbili. Mifano iliyooneshwa na vijana wengi waliopata nafasi za uongozi iwe katika chama au serikali hainishawishi kujenga imani juu yao. Kuanzia wakina Maige, Ngeleja, Nape, Mwigulu na wengine hasa UVCCM. Simaanishi wazee ndo suluhisho kwani wapo pia waliochemsha vibaya sana, lakini tunahitaji mfumo mzuri sana wa kumtathmini kiongozi.
 
Vijana walioko kwenye uongozi ambao tulikuwa na imani nao wametuangusha na wanazidi kuididimiza nchi hii. Hivi inakuaje kijana mwenye akili timamu kutumikia ufisadi? Hivi hatujui kwamba kizazi chakondokitapata shida miaka hijayo? Hivi unaona raha gani kusaliti wananchi wa Tanzania kisa kupewa pesa za kula na magari ya kutembelea? Hivi ni miaka mingapi utaishi hapa duniani kabla ya kufa? Hivi hao watoto na familia yako wakati hukiwa umekufa nao utawaachia husia kwamba wafanye mambo mabaya hili waendelee kuishi kama wakati ambao hupo hapa duniani?

Embu kijana wa kitanzania tufikirie sana sana. Leo nimesikia DW vijana wa Rwanda wameshindwa kupewa matokeo yao ya kidato cha sita kisa wamegoma kujiunga na M23. Wamekimbilia nchi jirani na pia wamesema wanatishiwa kuuliwa na wanausalama wa kwao kisa wamegoma kutumikia mambo ambayo hayana faida kwa wananchi wengine. Hivi sisi vijana wa Tanzania tunashindwa kukataa mambo kama hayo? Hivi kwenye nyumba za ibada tunaendaga kujionyesha kwa watu au tunakwenda kumwomba mungu? Mimi nazani wewe kama unashiriki kwa namna moja au nyingine ktk kuleta maisha ya mtanzania kuwa magumu jifikilie mara mbili mbili.

VIJANA WA TANZANIA TUBADILIKE, HII NI NCHI YETU SIO YA WATU WACHACHE, TUKATAE KUTUMIKA WAKATI MAMA, WATOTO, BABA, BABU, BIBI NA NDUGU ZETU WANAKUFA KWAKUKOSA MATIBABU YA HUAKIKA, VIJANA TUNAKOSA ELIMU BORA, HAKUNA MADAWATI, HAKUNA VITABU, WALIMU HAWAENDI KWENYE KOZI ZAO KUIMARISHA UJUZI, MAJI VIJIJINI HATA MIJINI BADO SHIDA, MAGONJWA YA KAWAIDA YANATUMALIZA, KILIMO BADO HAKIJA IMARIKA.

TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
mawazo yako makubwa sana, big up!
 
Back
Top Bottom