Vijana tubadilike

Wewe uliyeleta huu uzi nashindwa kukuelewa! Unataka kama siyo vijana ni akina nani wasimamie mustakabali wa mambo ya taifa?? nadhani una lengo la makusudi kuleta huu uzi na pia naweza kusema kuwa hujitambui!!!

ninajitambua vizuri ndio maana nikakwambia vijana tusimame wenyewe na sio mpaka tushinikizwe na vyama vya siasa,

serikali ni yetu sote,na wala sio ya ccm wala chadema.
 

Mkuu maelezo kibao unajichosha tu. Ukweli hakuna mwanasiasa anayetizama kukusaidia mara ngapi wabunge wanalilia kura but hakuna kitu. Jimboni kwangu tushabadilisha wabunge kibao wa vyama tofauti lakin hamna jipya. Ukitaka maendeleo jitoe mwenyewe sio kumtazama mwanasiasa
 

Tanzania hata tungeloga hakuna kiongozi imara.
 
Huo ushauri ni mzuri sana kwa Mazuzu wa Bavicha.
Sijui kama wanajitambua.

Kama kuna watu wasio na akili na wewe ni moja wapo! Thread hii inatoka pale Lumumba mambo ya sizitaki mbichi hizi baada ya kuona vijana hawana muda na ccm kwa sasa! Wewe na mwenzako mnataka tuache kufatilia siasa tumwachie nani? MaCcm? Hamnazo nyie! Kwanza baada ya kuwahamasisha vijana sasa tunahamia kwa mama zetu tutawanunulia kanga na vitambaa vya chadema maana mmewafanya mazuzu miaka 50 ya uhuru! Mimi wazazi wangu nimewapiga stop kushabikia ccm kule kijini na kama watakiuka basi na mimi sipeleki msaada maana mimi naumia kutafuta chakula nakatwa kodi kubwa lakini hamna huduma yoyote wanayopewa wazazi wangu huko kijijini! Nimewambia 2014/2015 ni chadema na kama hawaitaki basi wasiende kupiga kura kabisa lasivyo tutaonana wabaya ebo!


Tuitoe kwanza CCM ndiyo vijana tuache siasa baada ya nchi kuwa kwenye mikono salama! Hata chadema wakiharimu tunawatoa tu maana ni lazima tuwe na uongozi unaowaheshimu wananchi kwanza! Katiba mpya itakuwa hamna cha kusubiri mpaka miaka mitano ni immediate ukichemka unawekwa pembeni! Vijana ndiyo nguvu ya taifa lolote wasiposhiriki kwenye siasa nani sasa atafanya maana maana maendeleo ya nchi za kidemokrasia yanaletwa na siasa! Kasome vitabu vya mwlimu kuhusu ili tuendelee tunahitaji nini utakuta ni siasa safi na uongozi bora. Tatitzo la tanzania tumekosa hivi vitu kwa sababu ya ccm uongozi zero siasa chafu kila siku sasa utaendelea wapi! Nilazima ccm ipishe wajaribu na wengine na vijana ndiyo tutakao ifulumusha ccm kwa taarifa yako! Nyie endeleeni kuchukua buku saba pale lumumba sisi tunasongambele hatuachi siasa mpaka ccm kwanza itupishe wajaribu wengine ebo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…